Wanasiasa na wanaharakati hamasisheni wananchi waweze kujilimia chakula la sivyo hali itakuwa mbaya sana baadaye

Wanasiasa na wanaharakati hamasisheni wananchi waweze kujilimia chakula la sivyo hali itakuwa mbaya sana baadaye

SOEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2023
Posts
407
Reaction score
183
Nasema na wanasiasa na wanaojiita wanaharakati tuna jambo kubwa sana kwa wakati huu kama nchi kukosekana kwa mvua ya kutosha ambayo tunategemea kwenye kilimo ukiwemo na umeme

Hoja yangu ni hii mtumie majukwaa kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii na hata kwa hizi mvua chache hamasisheni wananchi waweze kujilimia chakula lasivyo hali itakua mbaya sana baadae .

Katiba muhimu sana lakini tusisahau mambo mengine ya maisha yanayoendelea hata tukiwa ndani ya katiba hii ! Katiba haileti chakula wala mvua hamasisheni wananchi wapande miti lakini pia wasilime kwenye vyanzo vya mji .

Elimu hii yote ni muhimu iwafikie wananchi na nyie mnanafasi kubwa sana kupeleka ujumbe huu kwa wananchi badala ya kukosoa tu serikali nk

Huwezi kuwa mwanaharakati ikiwa ukasimama katika kukosoa tu ! Kuelimisha na kuhamasisha wananchi katika maisha yao ya kila Siku ni muhimu zaidi na kazi za kiuharakati !

Upande wa afya pia tuelimishe wananchi badala ya kulalamika kwamba dawa hazipo tuelimishe pia juu ya kinga juu ya afya ! Mazoezi , Maji safi kuchemsha ya kunywa , chakula bora !!
 
Lema ameanza kampeni ya kuhamasisha Arusha wapande miti, iwe ya kijani.
 
Back
Top Bottom