mbona raisi wako ni mchumi mzuri tu
Ukiangalia hii nchi, mambo ya kiuchumi yanaenda ovyo sana.
Shilingi inazidi kushuka thamani, leo ni 1680 TSHS kwa DOla moja ya Marekani
Kilimo Kwanza imekuwa ni kelele tu na kuwapa mabeberu/mabepari ardhi ya Tanzania kwa kisingizio cha uwekezaji
Watu wanajali maendeleo ya vitu badala maendeleo ya watu
Siasa chafu ndo inatawala hii nchi
Wachumi wa Tanzania hii siwasikii hata wakiongea katika vyombo vya habari na kupaza sauti ama kutoa ushauri... Nchi hii kuna wachumi? Vyuo vikuu Mzumbe, UDSM, SUA e.t.c, Where are you?
Exactly brother!I agree with you.Kabla hujaanza kuwalaumu hao angalia hapa JF jukwaa linaloongoza kwa kutembelewa, jukwaa kama hili ambalo kwa asilimia themanini kama siyo tisini linaweza kumsaidia kijana kujikwamua kimaisha linatembelewaje ukilinganisha na jukwaa la siasa.
Ni ukweli kuwa waTanzania wengi tu ni makanjanja. Wanachojali ni kuwa na karatasi (vyeti) na kujipachika sifa za kisomi(Profesa, Dr.) lakini kivitendo ni kama shule ya msingi. Ushahidi nenda kwenye maktaba za vyuo vikuu uangalie ni asilimia ngapi ya vitabu/machapisho ni vya wasomi wa ndani. Ndogo mno. Si wasomi wa vyuoni tu hata makazini utendaji hauendani na sifa walizonazo wataalamu wetu. Hali ni hivyo kwa wataalamu wa kilimo, madaktari, mainjinia, n.k. Nahisi mfumo wa elimu unahusika kwa kiasi kikubwa.Kabla hujaanza kuwalaumu hao angalia hapa JF jukwaa linaloongoza kwa kutembelewa, jukwaa kama hili ambalo kwa asilimia themanini kama siyo tisini linaweza kumsaidia kijana kujikwamua kimaisha linatembelewaje ukilinganisha na jukwaa la siasa.