Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
mjinga ndiye anayeweza kufundishwa apige kura gani, na mjinga ndiye anayedhani anaweza kumfundisha mwananchi mwenzake kura yake iweje.
mwelevu yeyote anatambua kuwa kila mwananchi ana maamuzi yake juu ya katiba.
kama anaona katiba imekidhi au haijakidhi basi anapiga kura na matokeo ya kura ndiyo yataamua kama katiba ifanyiwe marekebisho kwa maana wananchi wameikataa kuwa kuna mambo ya muhimu hayajawekwa au iko vizuri kwa maana kila kitu wananchokihitaji wananchi kimewekwa na imebaki utekelezaji tu.
kila mwananchi anafanya maamuzi yake labda mjinga wa kuelewa ndiye anasaidiwa na wenzake kuweka dole la ndio au hapana.
Katiba mpya itapigiwa kura na watanzania wapenda amani na wazalendo,licha ya kuwepo kwa upinzani wa wachache ambao hawajawahi hata kuisoma!