Wanasiasa walivyo wanafiki, sasa Raila hasemi kuhusu uchaguzi wa jana

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Uchaguzi wa marudio umetendeka jana kwenye eneo bunge la Kitutu Chache, ambao uliendeshwa na IEBC, ambapo mgombea ambaye alikua anapigiwa debe na Raila ameibuka mshindi na kutunukiwa ubunge. Ikumbukwe kwamba huyu mgombea ni wa chama kingine, kwani Raila alitelekeza mgombea wa chama chake ODM na kumpigia debe huyu wa chama tofauti na chake.

Suala la msingi, walijitokeza watu wachache sana, asilimia 37% ya wapiga kura wa eneo hilo, inaeleweka ni kwa ajili ya sababu nyingi, zikiwemo kwamba kama kawaida kura za marudio huwa hazivutii wapiga kura wengi.

Swali je, mbona Raila hakujitokeza na kubeza kama alivyofanya kwenye uchaguzi wa tarehe 26 ambapo alisema watu waligoma kujitokeza kwa kufuata maagizo yake. Na kwamba uchaguzi wenye wapiga kura wachache hauna uhalali/legitimacy. Wanasiasa ni wanafiki sana, hubadilisha na kubadilika kama kinyonga.
--------------------------------------------------------------------------------------------

Ford Kenya's Richard Onyonka has retained his seat after emerging the winner in the just concluded Kitutu Chache South Constituency elections.

Onyonka defeated six opponents to clinch the seat with 10,122 votes.

Antony Kibagendi of Jubilee was second with 5, 074 votes while ODM's Samwel Omwando came a distant third with 4,324 votes.

Onyonka's supporters broke into songs of praise, cheers and jubilations after the results were officially announced by the constituency RO Hildah Imbo at St. Marys Mosocho Girls primary boarding.

The constituency has a total of 59, 017 votes but those who turned out to vote were 22,240 representing 37.40 percent.

Onkangi Kegoro of PDP and Justus Mochoge of ANC got 100 and 60 votes respectively.

The election was postponed from August 8 following the death of Jubilee Party candidate Leonard Mwamba on July 14.

Mwamba died in a road accident at Nyakoe along the Kisii-Kisumu road.

Jubilee Party later nominated Anthony Kibagendi to replace him
Ford Kenya's Richard Onyonka beats Jubilee's Kibagendi to retain Kitutu Chache seat
 
MK254, tatizo la Kenya sio wanasiasa kama mnavyojidanganya, tatizo ni ukabila tu, mkiachana na ukabila hautoona hiyo effect ya wanasiasa, mkiwa na ukabila kila kitu hakiwezi kwenda sawa, wanasiasa ni watu wanaotafuta maisha yao kama walivyokuwa wakoloni, chochote ambacho wanadhani kitawasaidia kutimiza lengo lao wao wanakitumia, lakuchekesha ni kwamba, jambo lilelile leo akiliona linamsaidia, wanaliunga mkono na kulitetea kwa nguvu zote, kesho yake jambo lilelile akiliona linamzuia kutimiza malengo yake, analipinga na kuona halifahi, mfano mzuri ni huyo Raila katika hili.

Huku Tanzania Lowasa alipokuwa CCM na mwenzake Somaye, walikuwa wanaitetea CCM kuliko walivyokuwa wakitetea Biblia, walipotoka CCM, wanavyoitukana CCM ni kama najisi.
 
A dimwit comment above by a perennial dimwit.🙄🙄
 
Sio kila kitu kinaanza na kuisha na ukabila Kenya, kuna mambo mengi sana nje ya ukabila na hili nimelisema mara nyingi japo tatizo huwa mumekaririshwa na hamutii bidii kwenye kujiongeza.

Zoezi la jana lilitendeka kwenye eneo bunge la Abagusii, sio kabila la Raila au hata Uhuru, hivyo kwenye upigaji kura wao wa ndani hawategemei ushawishi wowote wa kikabila. Wagombea ubunge na wapiga kura wote wametokea kwenye jamii hiyo.
 
Bado hujapata point yangu, na ninajua ni kwa sababu nimetaja neno kabila, jambo ambalo nimetonesha donda lako, mbona nimetolea mfano wa Lowasa na Somaye wakati wao sio trabilists?

My point ni kwamba, wanasiasa wako hivyo dunia nzima, wala sio Raila peke yake, kila mtu atatumia every resources available to achieve his/her goals. Lakini mkiwa hamna ukabila na mkabaki kupiga siasa za barabarani kama huku kwetu, hiyo effect ya Raila kusimamisha nchi nzima isongetokea, kwasababu wanasiasa leo wako huku, kesho wako kule, kama Lowasa juzi alikuwa CCM leo Chadema, huwezi jua kesho atakuwa wapi. Pambaneni na ukabila acheni ukaidi usiokuwa na tija.
 
Narudia tena sio kila kitu kinaanza na ukabila na kuisha na ukabila Kenya. Ni kweli ukabila upo, tena sana hilo halipingiki na hatuoni ufumbuzi wa suluhu itakayotegemewa hivi karibuni, tumeishi na donda la ukabila kuanzia hata kabla ya kupata uhuru, na tumeendekeza mpaka leo na jambo la kuhuzunisha tunapokeza hadi na watoto wetu. Hivyo hilo nakiri kama litakufurahisha kwamba nimekiri sawa.

Hata hivyo maisha yapo yanasonga kila siku, hapa nilipo kuna mradi nafanya na jamaa Mjaluo, Mkalenjin na Mluhya, hatuna issue kabisa na tena tunahusiana vizuri tu na kwa ufanisi mkubwa wa desturi ya Kikenya.

Hoja yangu ni kwamba wanasiasa, akiwemo Raila wana unafiki mkubwa sana, wanaishi kugeuza geuza kauli zao bila hata aibu. Ndio wote hutumia ukabila kupata kura, lakini pia wana mbinu zingine nyingi hata ukiondoa ukabila, kumbuka wanasklizwa pia na watu wasio wa kabila lao.
 
Hiwezu kulingamisha uchaguzi wa jimbo moja na uchaguzi wa wa rais, ni mambo mawili tofauti.
 
Narudia tena sio kila kitu kinaanza na ukabila na kuisha na ukabila Kenya. Ni kweli ukabila upo, tena sana hilo halipingiki na hatuoni ufumbuzi wa suluhu itakayotegemewa hivi karibuni, tumeishi na donda la ukabila kuanzia hata kabla ya kupata uhuru, na tumeendekeza mpaka leo na jambo la kuhuzunisha tunapokeza hadi na watoto wetu. Hivyo hilo nakiri kama litakufurahisha kwamba nimekiri sawa.

Hata hivyo maisha yapo yanasonga kila siku, hapa nilipo kuna mradi nafanya na jamaa Mjaluo, Mkalenjin na Mluhya, hatuna issue kabisa na tena tunahusiana vizuri tu na kwa ufanisi mkubwa wa desturi ya Kikenya.

Hoja yangu ni kwamba wanasiasa, akiwemo Raila wana unafiki mkubwa sana, wanaishi kugeuza geuza kauli zao bila hata aibu. Ndio wote hutumia ukabila kupata kura, lakini pia wana mbinu zingine nyingi hata ukiondoa ukabila, kumbuka wanasklizwa pia na watu wasio wa kabila lao.
Sasa hivyo unavyoishi na wajaluo na makabila mengine ndivyo inavyopaswa kuishi hivyo hata katika kipindi cha uchaguzi, lakini siku ya kupiga kura ya rais, kila mtu anarudi kwenye kabila lake kuogopa vurugu.

Kitu kinachoniogopesha ni kuona kwamba, ukabila umeathiri uwezi wa wakenya wengi katika kufikiria logically, kama mtu ni mjaluo, basi lolote analofanya Raila ni sawa na hakuna wa kumpinga au kujiuliza, na wakikuyu watapinga kila kinachofanywa na raila, na kinyume chake kwa Uhuru Kenyatta, hii ni hatari kubwa sana, ukiangalia serikali ya jubilee kwa sasa ilivyojaza watendaji wengi kuanzia ngazi ya katibu wakuu, wakurugenzi, na mameneja, toka kabila moja au mbili, ni wazi kabisa hapatakuwa na ufanisi katika utendaji wa kazi zaidi ni kulindana na kuoneana huruma.
 
Tatizo la Kenya na Afrika na kama ilivyo Tanzania ni kitu tunaita sycophancy, kumfuata mtu mmoja hata akifanya makosa tunasifia tu.

Leo hii hata kule Ujaluoni au hata Ukikuyuni akiibuka mtu mwengine mwenye busara zaidi ya Raila au Uhuru hatosklizwa. Wameibuka wengi, wenye kutiririka mambo yenye hekima na busara ndani ya hayo makabila, lakini kwamba hawaendani na hao viongozi wawili inaishia hawaskilizwi kabisa.

Ndio kama leo Tanzania hapo, japo nyie hampo kwenye makundi ya Kikabila lakini uozo unabaki ule ule, nimeshuhudia mijadala ya Watanzania hata wasomi, ambao wanabisha kila kitu anachokifanya Magufuli na pia nimewaona wanaosifia kila kitu chake. Unakuta mtu hafikirii logically kabisa, hata kama akiletewa kila aina ya taarifa au ushahidi.
 
Back
Top Bottom