Wanasiasa wanatuua mapema. Pesa za NSSF wanazitumia kwa maslahi yao, jamani tupige kelele

Wanasiasa wanatuua mapema. Pesa za NSSF wanazitumia kwa maslahi yao, jamani tupige kelele

bob nasta

Senior Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
145
Reaction score
118
Tupige kelele hadi masikio yawaume tuko kimya sana jamani .nendeni kwenye ofisi za NSSF mkaone watu walivyokata tamaa na maisha yani afadhali mkoloni.

Mtu unaangaika miaka labda 20 anakatwa mshahara wake huo mdogo,sasa akifika kule ataahidiwa mpaka atakufa njaa.

Vijana mko wapi mbona waoga wazee wenu tunakufa mnatuona ni kundi la watu wachache tu wanacheza na akili zetu. Tusaidieni kupiga kelele ikiwezekana kila siku tulalamikie hili jambo.

Tunakufa jamani, mjue hata nyie ni wazee wa baadaye. Anzeni sasa kuweka sawa aya mambo, mtalia.
 
Sawa maajuza tuko wengi vipi wazee kule kijijini au wao hajawa maajuza acha kuweka mzaa kwenye jambo linalogusa maisha kama ilo
Pambana na hali yako shaibu usitake dunia nzima ikuonee huruma.
 
Watu wanateseka sana! Huyu Kawe Alumni ni mpuuzi fulani hivi! Watu wamestaafu mpaka wamefariki hakuna mafao. Takataka kabisa!
 
Hujaeleza pesa zinaliwa vipi na wewe una tatizo gani
 
Mchagueni Lissu muepuke haya mateso ya kuwa watumwa kwenye ardhi yenu.

Sent from my SM-J730GM using JamiiForums mobile app
Sijasema hela zinaliwa nimesema watu hawapewi pesa zao kuhusu mimi sio lazima niwe mimi watu ninaowajua wengi wanasafa ndo mana nasema tupige kelele labda na sisi tukifika uko kutakua na urahisi
 
PSSSF na NSSF Hawana Pesa?

Wabunge wa CCM wanazitumia kuchapisha Mabango?
 
Psssf hali ngumu,miaka 4 wanazungusha wastaafu tu.

Pesa hakuna?
 
Back
Top Bottom