Wanasiasa wanavyotumia dini kuwanyonya/kuwakandamiza raia

Wanasiasa wanavyotumia dini kuwanyonya/kuwakandamiza raia

Burkinabe

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2023
Posts
2,354
Reaction score
4,024
1. Eti msichanganye dini na siasa wakati kwenye misaafu tunasoma dini na siasa haviwezi kutenganishwa. Na ndiyo maana viongozi wetu huapa kwa misaafu hiyo.

2. Eti viongozi wa dini wanapaswa kuwafundisha waamini wao Unyenyekevu na utii kwa mamlaka (serikali) hata kama inawanyanyasa! Hii siyo kweli, maandiko hayafundishi watu kuwa wajinga. Na ndiyo maana katika baadhi ya maandiko ya misaafu, inasema jino kwa jino, jicho kwa jicho n.k. kwa maana kwamba mtu akileta ujinga na upumbavu alipwe kwa kadri alivyofanya. Hivyo kama kiongozi anadiriki kuwadharau raia wake hata kama hawakumchagua, ni vema na haki kwa raia pia kumdharau kiongozi huyo tena ikiwezekana kumtoa kabisa katika nafasi yake ya uongozi. Maana kiongozi yupo kwa ajili ya kuwawakilisha na kusikiliza kile raia wake wanasema na kufuata matakwa yao.

3. Eti, ufalme wao (maaskofu na viongozi wengine wa dini pamoja na waamini wao) uko mbinguni, kwa hiyo hawapaswi kujishughulisha na mambo ya hapa duniani! Huu nao ni upotoshaji maana maandiko wanasema mbingu na nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana (Mwenyezi Mungu). Hivyo viongozi wa dini wanapaswa kuhakikisha mambo ya waamini wao yanakwenda vizuri kuanzia hapa duniani hadi Mbinguni. Hivyo hapa napo wanasiasa muache ujinga.

4. Eti ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu, hivyo viongozi wa dini wasijadili lolote kuhusiana na siasa kwa sababu hayo ni ya Kaisari!

wadau, hizo ni kauli chache kati ya nyingi ambazo wanasiasa wapumbavu huzitumia for granted kuwanyonya/kuwakandamiza raia wao. Ni kweli dini inapaswa kuwafundisha watu kuwa na upendo, wapole wanyenyekevu, watii, wavumilivu n.k. Lakini pale ambapo kuna uonevu, ufisadi, na uovu uwao wote, wanapaswa kukemea pasipo uoga kwa sababu uoga ni dhambi ambayo itazuia wengi kutoingia Mbinguni siku ya kiyama!
 
Back
Top Bottom