Wanasiasa wanawake wana cha kujifunza na kujivunia kwa hawa wachache

Wanasiasa wanawake wana cha kujifunza na kujivunia kwa hawa wachache

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Uthubutu wao, utashi wao kamili wa kisiasa, ujasiri katika kujisimamia na kusimamia wengine, umakini wao katika kujipambania na kupambania wengine, uvumilivu wao na subra kwenye mazingira ya vitisho, dhuluma, dhihaka au manyanyaso ya aina zote katika mambo mbalimbali ambayo waliona ni uhuru na haki zao za msingi kuzitetea na kuwatetea wengine, ni kitu muhim sana kujifunza..

Misimamo yao isiyo tetereka wala kuyumba katika yale yote wanayoyaamini, na kwamba ni wajibu wao kuyatetea na kuyasemea bayana, kinagaubaga, kwa manufaa ya wanawake wote na maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla, ni jambo zuri sana la kizalendo kujifunza..

Umahiri wa kuibua na kujenga hoja, bila hofu, wala woga, bidii, ubunifu na moyo wa kutokukata tamaa, wala kuchoka kupambana, imekua ni somo muhimu sana kwa wanawake wote humu nchini.

Mh.Halima James Mdee(mb) na wenzake wote wa upinzani waliopo mjengoni, wanafanya kazi nzuri sana, watafika mbali sana kisiasa tuendako. Ujasiri na uvumilivu wa hawa ni darasa la kipekee sana kwa wanawake...

Ni fahari kama Taifa, kua na Rais madhubuti sana mwanamke Dr Samia Suluhu Hassan, lakini pia kua na wabunge makini, na mahiri sana wanawake, kama hawa kwa uchache..

Hakika, wanawake hawa, wameonyesha na kudhihirisha kwa umma, uwezo mkubwa wa wanawake katika uongozi, wamelinda heshima, haki na utu wa mwanamke katika jamii.

ama kwa hakika wamabainisha kwamba, wanawake wanaweza.

Kwa Pamoja Tunasonga Mbele Kulijenga Taifa 🐒
 
Back
Top Bottom