Pre GE2025 Wanasiasa wangekuwa wanapiga kazi muda wote kama ilivyo kipindi cha uchaguzi Tanzania ingekuwa wapi kimaendeleo?

Pre GE2025 Wanasiasa wangekuwa wanapiga kazi muda wote kama ilivyo kipindi cha uchaguzi Tanzania ingekuwa wapi kimaendeleo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Wote tunashuhudia kipindi hiki cha uchaguzi wanasiasa wakiangahaika huku na hukokuonesha wananchi wao ni watu wa kazi, wanawasikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati, wanafika mitaani kuangalia mambo yanavyoenda, ziara za kushtukiza zinapigwa kwelikweli, wengine mpaka wameweka utaratibu wa kuzunguka usiku kucha ili kuhakikisha kama kweli wananchi wapata huduma stahiki.

Tunajua hii ni danganya toto na kujiosha kipindi hiki ili wachaguliwe tena halafu watutelekeze kama kawaida. Huu ndio muda wa kuwaona wabunge majimboni mwao, kabla unaweza kufikiri wote ni wabunge wa Dar 😀 😀

Sasa vipi kama hii ndio ingekuwa hali ya kawaida (ambayo ndio actually inatakiwa kuwa)? Yaani viongozi wanapiga kazi namna hii, Tanzania ingekuaje kimaendeleo? Vipi kuhusu uwajibikaji wa viongozi? Habari za rushwa na ufisadi tungezisikia?

Vipi kuhusu huduma za maji na DAWASA? Madaraja na barabara mbovu tunazopigia kelele kila siku? Bei za huduma muhimu zingekuwaje? Upande wa Kodi je, bado zingekuwa zinaanzishwa kwa utitiri au hali ingekuwa tofauti?

Ingekuwa vipi hali ingekuwa hivi wakuu?

johnthebaptist Lucas Mwashambwa Kiranga Mshana Jr Erythrocyte Tlaatlaah Pascal Mayalla Benjamini Netanyahu FaizaFoxy Malaria 2 JokaKuu
 
Back
Top Bottom