Wanasiasa wapo CCM huwezi kuwa chama cha upinzani Afrika ukajiita Mwanasiasa. Wewe ni mwanaharakati tuu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Salama kabisa!

Inashangaza Sana. Au ndio Elimu za kikasuku. ELIMU za kukariri. Unakuta mtu na elimu yake Kabisa umri umeenda lakini anashindwa kutofautisha Mwanasiasa na Mwanaharakati. Anashindwa kuelewa MUKTADHA WA mtu kuwa mwanasiasa na kuwa Mwanaharakati.

Kwa mazingira ya nchi nyingi za Afrika, huwezi kuwa chama cha upinzani alafu ukajiita Mwanasiasa. Labda uwe na uelewa mdogo kuhusu hizo terminologies.

Wanasiasa ni watu ambao hufanya siasa kwenye nchi zenye uwanja sawa na HAKI Sawa katika shughuli zao za kisiasa.

Mfano, ukiwa chama tawala labda kwa hapa nchini Kwetu. Ukiwa CCM ni rahisi kufanya siasa na wewe utaitwa Mwanasiasa.

Ingawaje kuna mazingira ubabe katika siasa unaweza kutokea mfano Nafasi Fulani ndani ya chama kutolewa fomu Moja Jambo ambalo sio HAKI.

Lakini huwezi kuwa mwanachama wa vyama kama CHADEMA, sijui, ACT Wazalendo, n.k. alafu ujiite mwanasiasa. Huo ni uelewa mdogo.

Ikitokea mwanachama wa Upinzani Afrika akajiita mwanasiasa huyo anajaribu kueleza kuwa yeye ni mwanachama wa chama tawala iwe kwa kujua au kutokujua.

Kifalsafa, na kimantiki, na kihaki, Mwanachama wa upinzani Kwa nchi Zetu huyo ni mwanaharakati.

Kwa Sababu, vyama vya upinzani havina Haki Sawa mbele ya chama tawala. Na hii hufanya vyama pinzani kupigania baadhi ya HAKI ambazo hawana ili wawe Sawa na chama tawala. Huko kupigania hizo Haki ndiko kunawafanya waitwe Wanaharakati.

Narudia, niwatu wenye uelewa mdogo wa mambo ambao huwaita wapinzani wanasiasa ilhali sio wanasiasa Bali wanaharakati.

Pakiwa na tume Huru ya uchaguzi, Katiba na Sheria zisizopendelea chama chochote Basi hapo ndipo tunaweza waita wapinzani Wanasiasa.

Mtu ambaye anayefanya siasa na yupo chama cha upinzani huyo ni chama tawala logically(kifalsafa).

Acha nipumzike sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…