Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwa muda Mrefu mimi binafsi na wasomi wengine tumejitahidi humu na kwingineko kuelekeza na kuonya kwamba, hakuna haja yoyote kwa Wanasiasa kujichomeka kwenye soka na kuvitumia Vilabu vya soka kuosha nyota zao.
Wanasiasa wanayo maeneo yao mengi sana ya kusafishia nyota zao, wewe kama ni mwanasiasa na hasa uliye madarakani ukitaka kusafisha nyota yako, tenda mema kwa jamii, lete maendeleo kwa watu wote, linda katiba ya nchi, achana na Chawa, jari walio chini yako, Hakikisha maslahi ya Wafanyakazi yameboreshwa, ongeza Ajira.
Ukifanya hivi hutahitaji umaarufu wa bei rahisi wa kuingia kwenye soka, huku hujui hata danadana zinavyopigwa. Haya matamasha ya Simba na Yanga hayana uadilifu wowote, yamejaa nyimbo, muziki na maneno ya kejeli yaliyojaa matusi ndani yake (Jikumbushe tamasha la Yanga la juzi).
Kwa kiongozi yeyote anayejiamini hana sababu yoyote ya kushiriki matamasha haya yenye uchafu ili ajipatie umaarufu.
Napinga Rais kushiriki matamasha kama haya, hii ni kwa sababu yamejaa uhasama, hili likifanyika iitaleta mgongano baina ya Mahasimu wa vilabu vyote viwili.