Wanasiasa wasitumie vilabu vya soka kujipatia umaarufu wa bure

Wanasiasa wasitumie vilabu vya soka kujipatia umaarufu wa bure

Leo nitatowa ufafanuzi wa mwisho asiyetaka kuelewa na aweke pamba masikioni.

Kimsingi wengi wanajuwa club ya Yanga ndio iliyotumika na Tanu kama cover ya wapigania Uhuru, hili halihitaji maelezo.

Club ya Sunderland ilikuwa inamilikiwa na Waarabu serikali ikawapora Waarabu timu na kuipa jina la Simba (Kawawa Simba wa vita) hii ndio code ya timu kwa wasiojuwa.

Makao makuu ya Yanga Jangwani na makao makuu ya Simba Msimbazi pesa za Ujenzi ametowa marehemu Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar.

Sasa kwa kifupi hizi timu ni za serikali hizi kabla hazijaingia madarakani.

Hakuna muhindi yeyote, Mwarabu wala Persian anayeweza kumiliki hizi timu. Ni za serikali kwa 100% wanazitumia kwa wakati wanaohitaji wao.

Hawa Wahindi na Waarabu mnaowaona Simba na Yanga wameachiwa fursa tu ya kutumia hizo brand kibiashara na wahakikishe wanaingiza pesa na siyo serikali itowe pesa zake.

Michakato mingine yote unayoiona ya kimfumo Simba na Yanga ni kiini macho tu, Mo Dewji muda wake ukifika ataondoka ataiacha Simba na GSM mwisho wake ukifika ataiacha Yanga.

Mwisho wa kiini macho hiki ni siku Ccm itakapofurumushwa madarakani ndio mtayajuwa mengi msiyoyajuwa na ndio mtaelewa kwa nini Ccm ilikuwa haitaki kutoka madarakani, hapo ndio timu kama Singida Fountain na Azzam wanaweza kufurukuta kwenye fair competition.
Bonge la ukweli
 
Kwa muda Mrefu mimi binafsi na wasomi wengine tumejitahidi humu na kwingineko kuelekeza na kuonya kwamba, hakuna haja yoyote kwa Wanasiasa kujichomeka kwenye soka na kuvitumia Vilabu vya soka kuosha nyota zao.

Wanasiasa wanayo maeneo yao mengi sana ya kusafishia nyota zao, wewe kama ni mwanasiasa na hasa uliye madarakani ukitaka kusafisha nyota yako, tenda mema kwa jamii, lete maendeleo kwa watu wote, linda katiba ya nchi, achana na Chawa, jari walio chini yako, Hakikisha maslahi ya Wafanyakazi yameboreshwa, ongeza Ajira.

Ukifanya hivi hutahitaji umaarufu wa bei rahisi wa kuingia kwenye soka, huku hujui hata danadana zinavyopigwa. Haya matamasha ya Simba na Yanga hayana uadilifu wowote, yamejaa nyimbo, muziki na maneno ya kejeli yaliyojaa matusi ndani yake (Jikumbushe tamasha la Yanga la juzi).

Kwa kiongozi yeyote anayejiamini hana sababu yoyote ya kushiriki matamasha haya yenye uchafu ili ajipatie umaarufu.

Napinga Rais kushiriki matamasha kama haya, hii ni kwa sababu yamejaa uhasama, hili likifanyika iitaleta mgongano baina ya Mahasimu wa vilabu vyote viwili.

View attachment 2709257
Pumbavu kwa hiyo unataka kumpangia rais cha kufanya

Kampangie mke wako

wacha rais ajichanganye na raia apendavyo.
 
Mwanasiasa anatumia kila fursa anayoiona itampaisha kwenye siasa zake.kikubwa wengine waache kualalamika tu watumie fursa kama hizi.
 
Back
Top Bottom