Wanasimba na Benchikha sasa ni damu damu

Wanasimba na Benchikha sasa ni damu damu

Best Daddy

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
950
Reaction score
1,672
Kutokana falsafa yake wakati anaiongoza RS Berkane, USM Alger(Timu pekee nilizomfuatilia) nilikua na ukakasi wa mapokezi ya falsafa ya Benchikha kwa wanasimba. Lakini niweke wazi, Once facts change, I change too.

Japo ni mapema kuyasema haya, lakini wahenga mnasema nyota njema huonekana asubuhi. Wanasimba wamempokea Benchikha kwa mikono miwili and with their open heart, kitu ambacho Robertinho alikikosa kuanzia ngazi za baadhi ya viongozi(Rejea kauli za Mzee Dewji) na Mashabiki(soon alipofanya Sub ya Chama, na baadae objective ball haikupendwa na wengi).

Hii hitimisho yangu imetokana na kupitia baadhi ya maoni ya mashabiki wa Simba katika mitandao ya kijamii. Haya maoni hasa yamechagizwa na hizi mechi mbili alizosimamia, Ile ya Jwaneng Galaxy na hii ya Wydad Casablanca pale Marrakech.

Ukitoa Surprise yake kwangu ya kubadili mfumo wake pendwa 4-2-3-1 hadi 4-4-2 (Japo hana Striker wa maana wa kumsaidia baleke) ila wote tumeshuhudia anaonekana hajaja Simba kufundisha "Haram Ball" labda hadi pale aina hii ya mpira itakapo hitajika katika mechi husika.

Tumeona improvement ya baadhi ya wachezaji katika maeneo kadhaa mfano Onana off-ball amekuwa bora sana, anajitahidi kukaba tofauti tulivyomzoea. Kanoute pia ubora umeongezeka kwake. Bila kusahau kuna mabadiliko makubwa kwa timu off-ball (Ikiwa haina mpira) sasa wanakaba na kuziba au ku-track mianya vizuri huku jitihada na physique za wachezaji zikiimarika. Pamoja na kukosa alama tatu katika mecho hizo ila kuna mabadiliko chanya katika kikosi.

Hivyo basi, Benchikha sio lazima utupe Joga Bonito(Play Beautiful) kama vijana wa Brazil. Sio lazima utupe Tiki - Taka kama ile ya Guardiola akiwa na Prime Barcelona. Sikupangii, ila ukikosa kosa ile total football ya vijana wa Amsterdam(Ajax) basi tupe tu Gegenpressing (Counter-Pressing). Japo ni mdogo kwako, ila sio mbaya ukatuletea kidogo anachokifanya Klopp pale Liverpool, au chungulia jangwani pale kuna vi-element fulani vya hii aina ya uchezaji.

N.B. Hapa nazungumzia aina ya uchezaji tu, simaanishi viwango au uwezo wa timu tajwa hapo juu.

Oh, nimeanza kutoa fikra zangu tena. Ila kubwa nililokuwa nazungumzia ni mapokezi chanya ya Benchikha kwenye mioyo ya wanasimba.

Ni mengi yamezungumzwa, ila siwezi nukuu wazo la kila mtu mmoja mmoja, kitu pekee naweza fanya kuyafupisha kama ifuatavyo:

Hapa tumepata kocha bora sana, viongozi tunataka mshikamane na Kocha ili ajenge simba iliyo bora. Na kwa nyakati zijazo mambo yasipoenda vizuri hatutaki kocha aguswe, muanze kutimuana wenyewe huko ofisini"~ Mwisho wa ufupisho wa maoni ya mashabiki wa Simba.

Kuna kauli nasikia mtaani kuwa Benchikha ni engine ya Fuso, ndani ya bajaji(Simba, lakini nitamaliza kwa kutoa faida kadhaa za kuwa na kocha mkubwa kama huyu katika timu zetu. Kubwa kabisa ataweza kutuletea outside perspective, maana tayari amepita sehemu ambazo zinatoa vitu vilivyo bora.

Tunaweza ona baadhi ya vifaa vipya mazoezini, aina ya mazoezi mapya na hata Kupata urahisi hasa nyakati za usajili, maana wachezaji wengi ukitoa kigezo cha pesa au ukubwa na vison ya timu, basi aina na ukubwa wa mwalimu huvutia wachezaji sana katika timu husika.

Bila kusahau hata "Mangungu au Jaribu tena hawezi mpangia kikosi mwalimu wa daraja hili. "Haha utani". Ila Kikubwa Simba itanufaika na mengi sana kuanzia ofisini hadi kwenye pitch.

Yote ya Yote, ukanda huu wa CECAFA tumepata makocha bora wawili hadi sasa ambao ni Benchikha wa Simba Sports Club na Florent Ibengé. Hawa makocha wanaweza upeleka ukanda huu sehemu bora sana. Angalia Ibenge anavyoipika Al Hilal, pamoja na kuwa hawachezi league zao, ila performance ni bora sana. Huu sio upendeleo, ila kuna baadhi ya makocha japo sio wabaya ila bado nashikwa na kigugumizi juu ya mienendo yao katika mechi husika.
 
Kocha hata mwezi bado, mnajifanya unajua uchambuzi. Unachokiona jana ni wachezaji wa Simba kuamua kupambana kumshawishi kocha mpya ili wapate namba. Robertinho alivyokuja Simba uliona wachezaji walivyokuwa?
 
Kutokana falsafa yake wakati anaiongoza RS Berkane, USM Alger(Timu pekee nilizomfuatilia) nilikua na ukakasi wa mapokezi ya falsafa ya Benchikha kwa wanasimba. Lakini niweke wazi, Once facts change, I change too.
na kigugumizi juu ya mienendo yao katika mechi husika.
Simba vs Al Ahly ulikuja na uchambuzi kusifia uchezaji wa Simba, na ile ndio performance ya wachezaji wa Simba wakiamua kujitoa kupambana, ni sawa na sasa wanavyopambana kumshawishi kocha. Ila haitochukua muda watarudi katika utaratibu wao
 
Ni suala tu la muda kabla hamjaanza kumpigia makelele kama mlivyofanya kwa watangulizi wake. Mna nongwa sana nyinyi.
Labda inaweza tokea kwa hapo baadae, ila kwa sasa wakati ambao kuna baadhi ya mambo chanya yanaonekana katika timu sio mbaya akapongezwa.

Tofauti ya watangulizi wake hasa Zolan na Robertinho, Benchikha amekubalika mapema sana na mashabiki wengi wa Simba.
 
Kocha hata mwezi bado, mnajifanya unajua uchambuzi. Unachokiona jana ni wachezaji wa Simba kuamua kupambana kumshawishi kocha mpya ili wapate namba. Robertinho alivyokuja Simba uliona wachezaji walivyokuwa?
Unaweza ukawa sahihi, Ila binafsi nimeona improvement kwenye timu tofauti na mechi zilizopita.

Hii ni tofauti na wakati wa Mr. Objevtive. Robertinho aliipokea Simba iliyokua inacheza soka safi kutoka kwa Guardiola "Mgunda", ila mechi yake ya kwanza kwa Mkapa dhidi ya Mbeya City (FT: 3-2).
Kauli pekee mtaani ilikua "if it ain't broke don't fix it". Maana Simba ilianza kama kujitafuta, kelele zilikua nyingi sana mtaani, wengi wakidai bora Mgunda achukue timu.
 
Simba ilikosa fitness kingine imejaa wachezaji wazee na usajili usiojali mapungufu. Ngoja tuone usajili wake kwanza hizi mechi za ascf zitamsaidia kujua wachezaji Ila Matola sijui anafanya Nini pale.
 
Simba ilikosa fitness kingine imejaa wachezaji wazee na usajili usiojali mapungufu. Ngoja tuone usajili wake kwanza hizi mechi za ascf zitamsaidia kujua wachezaji Ila Matola sijui anafanya Nini pale.
Kweli kabisa. Hofu yangu usajili utakua mgumu sana kama timu ita-qualify robo fainali. Aisee hapa timu nzima ya Scouting ijipange sana, maybe hata kwenda huko Latin America.

Maana baadhi ya wachezaji wazuri wanao-pointiwa tayari wameshiriki mashindano haya msimu huu.
 
Mimi ni Yanga damu damu Ila nawashauri Simba SC Msije kumuondoa huyu kocha wenu haijarishi mtaishia makundi

Ushauri ni bure
 
Back
Top Bottom