Wanasoka wenye uwezo wa kawaida ila walibebwa na mafanikio ya timu zao

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Karibuni wana ukumbi,
Kuna wachezaji walikuwa/wana uwezo wa kawaida lakini wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na mafanikio ya timu aliyochezea/anayochezea.

Mfano:
Anderson enzi akiwa Man Utd ana medali 3 za EPL wakati uwezo wake ulikuwa ni wakawaida sana kulinganisha na mtu kama Steven Gerrard ambaye hana medali yoyote ya EPL.

Kiungo Christoph Kramer wa Borrusia Monchegladbach ana medali ya Kombe la Dunia aliyoshinda na Ujerumani mwaka 2014 licha ya uwezo wake wa kawaida.

Victor Valdes ameshinda kila aina ya taji katika soka akiwa na Barcelona na Hispania lakini uwezo wake ni wa kawaida sana.

Karibu uendelee...
 

mikael silvestre : 5 premier league + 1 uefa champions league (2008)

wes brown :5 premier league + 2 uefa champions league + 1 club world cup

roy carrol : 1 premier league.
Aigoooooo pale unapokwenda kuangalia mechi ya manchester united halafu unagundua alex ferguson hawa watu watatu amewaanzisha, nilikuwa nachukia sana.
 
M
Mikael sylvestee alikuwa na uwezo mkubwa sn....HUONI HADI babu wenger alimsajiri from manutd?
 
Unawezaje kusema Victor Valdes alikuwa wa kawaida wakat Barcelona ikishinda mataji mengi yeye ndoalikuwa analinda goli? Angekuwa mbovu angekuwa anaruhusu magoli mengi na hiyo barca isingeshinda mataji mengi katika kipindi chake.
 
Barcelona wachezaji most of them waliopita na wasasa uwezo wao ni wa kawaida sana mfano tu Neimar,semedo,vidal,gomes, alcacer and Digne, hawa wote ni wakawaida sana__so Mafanikio yao wameyapata kutoka kwa LEONEL MESSI__ bila Messi wasingepata mafanikio yoyote__

MESSI ndiye engine ya Barca, bila yeye BARCA si
chochote. So wamshukuru sana kiumbe huyu kuwahi kutokea
 
Messi asiye na ndevu alibebwa sana na timu hususani na viwango vilivyotukuka vya Xavi na Iniesta.

Messi Mandevu kaibeba timu juu ya mabega take akifanya mambo yaliyokuwa yakifanywa na watu watatu yaani yeye mwenyewe akiwa hana ndevu,xavi na iniesta Kwa wakati mmoja

Ajabu akiwa mchezaji Kamili zaidi na madevu juu ballon d or zimekimbia ila Nina hakika Messi hatakufa kabla hajachukua balloon d' or moja
 
Hapo ndo utajua mpira inawezekana uchawi unatumika. Golini Carol, mabeki Brown na Sylivestre!! Halafu mnashinda kiulaiini tena bao 5 na Tot?
 
Watanzania bwana wakimchukia mtu.....

Sasa unawezaje kusema kuwa mchezaji fulani ni mbovu hali ya kuwa na yeye ni miongoni mwa wachezaji wa kwenye hiyo waliyoleta mafanikio kwa juhudi zao.......

Labda tu niwakumbushe kuwa kwenye Timu kuna kila mchezaji ana nafasi yake uwanjani.....

Kuna viungo ,washambuliaji na walinzi..........

Kila mmoja anapotimiza wajibu kwenye timu na wote mkiwa na lengo moja ndio huzaa mafanikio ya timu.........

Mtu anayejuwa na ambaye angalau alishawahi kucheza mpira anajua naongelea nini......

Kocha anayetambua majukumu yake mpaka anaamua kukuweka kikosi cha kwanza maana yake ni kwamba unafaa kwa nafasi hiyo...........

Tatizo la waTanzania hawauchambui mchezo bali wanawachambua watu.......
 
Upo best
 
Messi ni wa kama kawaida sana kama Kakichuya tuuuu,sema timu inamneba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…