Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
Habari Leo
CHAMA cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) kimekiri kutoa waraka ambao wenyewe wameuita ‘tafakari' ukikishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukituhumu kuwa ndicho kikwazo cha ukuaji demokrasia nchini.
Waraka huo uliopewa jina la ‘Tafakari ya CPT, Uchaguzi Huru na Halali', umeishambulia CCM na kuitaja kuwa kikwazo cha demokrasia ndani ya vyama vya siasa visivyokuwa na nguvu kiuchumi.
Pia CCM imesema kwa sasa haina muda wa kujibizana na mtu au waraka wowote na badala yake inatumia dakika zilizobaki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, kufanya kazi kwa mujibu wa ilani yake.
Akizungumza na HabariLeo jana, Mwenyekiti wa CPT, Joseph Ibreck, alisema chama hicho hakina ugomvi na CCM isipokuwa kimetoa ‘tafakari' hiyo, kwa lengo la kushirikisha wananchi kutoa mawazo katika masuala yanayohusu mustakabali wa nchi. "Huu si waraka ni tafakari ambayo ni mwendelezo wa Ilani iliyotolewa na chama hiki kuhusu Uchaguzi Mkuu na tutaendelea kutoa tafakari kama hii hadi mwisho wa dunia," alisema Ibreck.
Alisema ‘tafakari' hiyo inalenga zaidi sheria ya gharama za uchaguzi iliyopitishwa hivi karibuni bungeni. "Lengo hapa ni kutaka kujua kwa nini sheria hii imekuja sasa, inamlenga nani, madhumuni ya gharama za uchaguzi ni nini na nani atafaidika."
Hata hivyo, alisema ‘tafakari' hiyo ilitoka muda mrefu kabla hata rasimu ya sheria ya uchaguzi haijaenda bungeni, lakini ilichelewa kutolewa na kusambazwa.
"Napenda ieleweke kuwa hatuna nia mbaya, tumewatumia CCM kwa kuwa wao ndio wanaotoa mapendekezo ya sheria, hatuna ugomvi nao."
Akizungumzia suala hilo, Chiligati alisema chama chake hakina muda wa kupoteza kujibizana na watu na kuwataka wenye malumbano dhidi ya CCM, wasubiri kampeni.
"Huu si wakati wake, wasitupotezee muda, tuko kazini na hatutaki malumbano na kundi lolote, maneno au malumbano yatafanywa wakati wa kampeni, ila wanaosema waacheni waendelee sisi tupo kazini," alisema Chiligati.
Alisema kama ni soka kwa sasa ni dakika za mwisho ambazo hazijaisha. "Tukiendekeza malumbano au maneno tutafanya kazi saa ngapi?"
Kwa upande wake, Makamba alipoulizwa alisema "hata kama waraka huo ukitufikia hatuna muda wa kujibu, ukweli ukitokea uongo utajitenga." Alikanusha tuhuma zilizotolewa dhidi ya CCM na kuongeza kuwa hakuna ujanja wowote unaotumiwa na chama hicho kujipatia mamlaka na katika suala la kujitwalia mali zisizohamishika na hisa, alisema mali zote ni za chama hicho.
Kwa mujibu wa waraka huo ambao umeshambulia CCM, pia unakosoa mwelekeo wa kisiasa nchini hasa baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa siasa ya vyama vingi miaka 18 iliyopita, ambapo pia umeitaka CCM kutangaza hesabu za gharama halisi zilizotumiwa na vyama vyote vya siasa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.