Sharedbusiness
Member
- Dec 15, 2018
- 6
- 5
TANZANIA SHARED BUSINESS (TSB)
BUSINESS PARTNERSHIP OPPORTUNITIESTanzania Shared Business (TSB) inatafuta washirika wa biashara katika kampuni ya kuzalisha unga wa sembe Songea na kusambaza kwenye masoko ya mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es salaam.
Angalizo: Kuepuka utapeli na kuvunja sheria hakuna sehemu yoyote unayotakiwa kumpa mtu pesa mpaka utaratibu wa kampuni utakapoanza baada ya kuhudhuria au kufanyika mkutano wa wadau katika mkoa wa Mtwara au Dar es salaam au Lindi au Songea. Mkutano huo utapitia na kupitisha mpango wa biashara na kutoa uelekeo wa mambo muhimu ya katiba na muundo wa kampuni.
1.0 UTANGULIZI
TSB imefanya utafiti na kubainisha ni namna gani mtu mmoja mmoja anakwama katika biashara na ujasiriamali kutokana na changamoto za mitaji, ukosefu wa uzoefu, taarifa na maarifa na changamoto za masoko.
Hivyo basi TSB imekusudia kuunganisha mitaji,uzoefu, maarifa,taarifa na uzoefu wa masoko na uendeshaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara kuanzisha kampuni za kuchakata mazao (agro proccessing businesses) na kuwezesha mtandao wa masoko na usambazaji wa bidhaa za vyakula. Kuanzisha Kampuni ya kuzalisha unga wa sembe mjini songea na kusambaza kwenye masoko ya Mtwara, Lindi na Dar es salaam ni uanzaji wa makampuni (group of companies) yaliyokusudia watanzania kujiunga na kuanzisha viwando vidogo hatimaye kumiliki uchumi na kuzalisha ajira.
2.0 MPANGO WA UTEKELEZAJI
Mpango wa biashara umeshaandaliwa na mdau ambaye yupo kwenye biashara husika pia ni mwanahisa mtarajiwa wa kwanza. Anahitajika mshirika mmoja tuu kwa kila wilaya kati ya wilaya 17 zifuatazo:
Mtwara,Masasi,Tandahimba,Nanyumbu,Newala,Lindi,Kilwa,Nachingwea,Ruangwa,Liwale,Songea,Mbinga,Ilala,Temeke,Kinondoni,Ubungo na Kigamboni.
Mshirika mmoja atakayepitishwa kutoka kila wilaya atakuwa mmiliki wa kampuni kwa kiwango cha mtaji atakachoshiriki kuanzia million tatu,pia atapata mafunzo na maelekezo mbali mbali. Pia mshirika atakuwa na jukumu la kuuza(marketing and sales) bidhaa husika kwenye wilaya aliyochagua na kupitishwa.
3.0 VIGEZO VYA KUWA MSHIRIKA
Kigezo a au b kama ifuatavyo;
(a)Awe tayari kuchangia million tatu au zaidi na moja ya vigezo vifuatavyo:
- Achague wilaya ambayo Atakuwa na haki na wajibu wa kutangaza na kuuza bidhaa husika au
- Awe mtaalamu wa uhasibu CPA (T) anayejua Kuandaa taarifa za fedha na kodi (Financial Statements and regulatory tax issues).
- Awe mtaalamu wa sheria za biashara au
- Awe na ujuzi wa technolojia ya chakula au
- Awe mtaalamu wa mitambo
(b)Mwenye mtaji kuanzia milioni sita anaweza kuwa muwekezaji anayesubiri faida bila kuhusika na shughuli yoyote ya kila siku.
4.0 JINSI YA KUOMBA KUWA MSHIRIKA
Muombaji anatakiwa kuandika barua akieleza kiasi anachoweza kuchangia kampuni , aeleze ujuzi au uzoefu alionao na kama yupo kipengele cha haki na wajibu wa kuuza aeleze katika eneo lake ni mikakati gani inaweza kusaidia kuuza bidhaa.
Barua yenye namba za simu itumwe kwa barua pepe kwa sharedbusiness84@gmail.com
TUKIUNGANISHA RASILIMALI NA MAARIFA TUTALETA MABADILIKO