Wanataka 150,000/= ili nipate hati ya nyumba

Pole mleta uzi, Kwa changamoto uliyo kutanana nayo. Naomba nikupe elimu kidogo;
Zoezi la Urasimishaji Makazi, kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali ni Kwamba Kila Mmiliki wa Ardhi atachangia Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini (150,000). Hii gharama itahusisha kazi zifuatazo;
1. Kutambua Mipaka ya Kiwanja/Eneo lako
2. Kuandaa Michoro ya Mipango Miji, Hii itaonesha Matumizi Mbalimbali ya Ardhi (Makazi, Biashara Shule n.k)
3. Kupima (Kuweka alama za Upimaji Ardhini, hapa ndio panahusisha zoezi la upandaji mawe maalumu ya Upimaji, kuonesha mipaka kati ya Kiwanja na Kiwanja au Kiwanja na Barabara).

Baada ya Haya mazoezi matatu kukamilika na Ramani zote kusajiliwa na Wizara (kiwanja kikapata namba, pamoja na Kitalu). Hapo ndio inakua Mwisho wa matumizi ya ile Laki Moja na Elfu Hamsini (150,000/=).

Kazi hizo nilizo zitaja hapo juu Zinaweza Fanywa na Wataalamu wa Ardhi kutoka Halmashauri Husika au Makampuni Binafsi.

Baada ya Kukamilika sasa kwa zoezi la Upangaji na Upimaji, zoezi linalofuata ni Umilikishaji. Hapa sasa kile kiwanja chako kinatakiwa kitengenezewe Hati.

Hati hazitolewi Bure; Kuna gharama ambazo mmiliki wa Kiwanja Anapaswa kuzilipa kwa Serikali ili aweze Kumilikishwa. Gharama za hati huwa hazilingani kama zile za Upangaji na Upimaji. Gharama za hati zinategemea Vitu vikubwa vitatu;
1. Ukubwa wa Kiwanja
2. Matumizi ya Kiwanja
3. Mahali kiwanja Kilipo.
Kwa mfano; Kiwanja cha makazi chenye ukubwa wa Mita za Mraba 1,000 kilichopo Katikati ya Mji, Gharama zake za hati hazita Fanana na Kiwanja Chenye ukubwa kama Huo ila matumizi yake ni Ya Biashara.

Kwa Kifupi;
Kuna Gharama za Upimaji na Gharama za Umilikishaji (Hati), tofauti kubwa Gharama sa Upangaji na Upimaji zinaweza Kulipwa hata kwa Kampuni Binafsi kupitia Akaunti za Benki.
Ila gharama za Hati zinalipwa Serikalini peke yake, Na siku izi malipo yote ya Serikali, ni lazima yafanyike kwa Control Number.

Mtoa mada Unaweza tumia huu kama Muongozo kutatua changamoto yako.
 
Nashukuru sana kwa maelezo mazuri kabisa ambayo yamenifungua pakubwa mno na nimejua pakuanzia , inamaana pindi ntakapo rudi ntawaomba wanipatie control number kwa ajili ya kufanya malipo . Ila ili pendeza vitu kama hivi wangekuwa wanatupa elimu kidogo na kwa kupitia haya maelezo ntakuwa mjumbe mzuri kwa wengine watakao kitana na sintofahamu kama yangu .
 
Kuna hati ya nyumba?
Nadhani ni hati ya urasimishaji wa makazi , nilikosa namna nzuri ya kuandika hapo ila ukisoma vizuri nahisi naweza kueleweka hasa nilikuwa nimemaanisha nini .
 
MImi nilitaka kurasimisha nyumba wilaya ya kibindoni nikaambiwa nilipe 650,000/=!
 
Hakuna rushwa mkuu.
Upimaji ardhi ulikuwa ni kama anasa kabla ya punguzo mkuu.

HIyo ya 150k ni ya upimaji tu tena ni punguzo kwani nusu ililipwa naserikalu.

Baada ya upimaji utaenda kulipia hati baada ya hesabu ya ukubwa wa kiwanja chako

Kama sio rushwa kwa nini hawatoi contro number
 
Ni kweli huu mfumo wa kulipia bank upo mkuu, sio huko pekee
 
Ukweli ni kuwa 150,000 haitoshi kabisa kupima na kupata hati, Mara nyingi wanawadanganya ili ukubali kupimiwa, wakikuambia mwanzon hadi upate hati ni Laki 5 utakimbia, ila ukishapata Ramani ya upimaji kwa laki na nusu, mbele mambo yanakuwa hivyo, na hiyo laki na nusu nyingine kama ni Dar haitoshi
 
Kama sio rushwa kwa nini hawatoi contro number
Hayo ni malipo ya Kampuni watakupa risiti, malipo ya serikali utapewa control number ambapo kuna reg fee ya certificate 50,000, Application 20,000, deed plan 20,000, Premium 0.5 ya market value, land rent, na reg fee
 
Yaani ni kutokufahamu tu, ingekuwa mimi ningeitoa hiyo laki na nusu chap tu kama ninayo, kikubwa wamenipa control number.

Post #21 ya mkuu Komba the Great kamaliza kila kitu.
 
Mimi pia moja kwa moja nilihisi kuna kitu hakipo sawa hapa , ila nikaona ngoja nisijitie ujuaji kwa kuwa kuna watu wanauelewa juu ya haya mambo ngoja niwashilikishe nijue undani wake

We mngoni acha kujifanya mjuaji. Hiyo pesa wanayotaka ni halali kabisa.
Waambie wakupe control number ukalipie
 
Uko sahihi mdau nami pia nililipa 120,000 ambapo niliambiwa ni gharama za upimaji. Baadaye nilipigiwa tena hesabu nyingine kulingana na ukubwa wa kiwanja na mpaka sasa nilishapewa hati
Mkuu, hiyo gharama uliyotozwa kulingana na ukubwa wa kiwanja ulilipa kwa 'control number' ama kwa mfumo upi?
 
Hati ya nyumba? Acha kusumbua JF nenda Halmashauri kaeleweshwe badala ya kutupigisha ramli humu
 
Mkuu, hiyo gharama uliyotozwa kulingana na ukubwa wa kiwanja ulilipa kwa 'control number' ama kwa mfumo upi?
Walicalculate wao wakanipa control namba kwenda kulipa ilikuwa kama 120,000 square mita 730
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…