Komba the Great
JF-Expert Member
- Apr 25, 2016
- 340
- 654
Pole mleta uzi, Kwa changamoto uliyo kutanana nayo. Naomba nikupe elimu kidogo;
Zoezi la Urasimishaji Makazi, kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali ni Kwamba Kila Mmiliki wa Ardhi atachangia Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini (150,000). Hii gharama itahusisha kazi zifuatazo;
1. Kutambua Mipaka ya Kiwanja/Eneo lako
2. Kuandaa Michoro ya Mipango Miji, Hii itaonesha Matumizi Mbalimbali ya Ardhi (Makazi, Biashara Shule n.k)
3. Kupima (Kuweka alama za Upimaji Ardhini, hapa ndio panahusisha zoezi la upandaji mawe maalumu ya Upimaji, kuonesha mipaka kati ya Kiwanja na Kiwanja au Kiwanja na Barabara).
Baada ya Haya mazoezi matatu kukamilika na Ramani zote kusajiliwa na Wizara (kiwanja kikapata namba, pamoja na Kitalu). Hapo ndio inakua Mwisho wa matumizi ya ile Laki Moja na Elfu Hamsini (150,000/=).
Kazi hizo nilizo zitaja hapo juu Zinaweza Fanywa na Wataalamu wa Ardhi kutoka Halmashauri Husika au Makampuni Binafsi.
Baada ya Kukamilika sasa kwa zoezi la Upangaji na Upimaji, zoezi linalofuata ni Umilikishaji. Hapa sasa kile kiwanja chako kinatakiwa kitengenezewe Hati.
Hati hazitolewi Bure; Kuna gharama ambazo mmiliki wa Kiwanja Anapaswa kuzilipa kwa Serikali ili aweze Kumilikishwa. Gharama za hati huwa hazilingani kama zile za Upangaji na Upimaji. Gharama za hati zinategemea Vitu vikubwa vitatu;
1. Ukubwa wa Kiwanja
2. Matumizi ya Kiwanja
3. Mahali kiwanja Kilipo.
Kwa mfano; Kiwanja cha makazi chenye ukubwa wa Mita za Mraba 1,000 kilichopo Katikati ya Mji, Gharama zake za hati hazita Fanana na Kiwanja Chenye ukubwa kama Huo ila matumizi yake ni Ya Biashara.
Kwa Kifupi;
Kuna Gharama za Upimaji na Gharama za Umilikishaji (Hati), tofauti kubwa Gharama sa Upangaji na Upimaji zinaweza Kulipwa hata kwa Kampuni Binafsi kupitia Akaunti za Benki.
Ila gharama za Hati zinalipwa Serikalini peke yake, Na siku izi malipo yote ya Serikali, ni lazima yafanyike kwa Control Number.
Mtoa mada Unaweza tumia huu kama Muongozo kutatua changamoto yako.