Wanatozo: Adui hufurahi akiona unateseka

Wanatozo: Adui hufurahi akiona unateseka

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Fikiria mfanyakazi anakatwa kodi PAYE kisha hela yake inaingia bank. Kule benki tena akitaka kutoa anakutana na kodi nyingine ya kikatili. Double Taxation.

Mfanyabiashara analipa kodi withholding tax na corporate tax. Bado haitoshi akitaka kufanya malipo benk anakatwa tozo.

Bado hicho kilichokatwa benki haitoshi. Chukua mshahara wako benki weka Mpesa umtumie mama yako kijijini. Unakatwa tozo kikatili. Bado hiyo cha mtoto, mama yako akitaka kutoa hiyo Mpesa anakatwa tozo.

Ni Mambo ya ovyo yanaendelea katika nchi hii, chini na Rais Samia na Waziri wake. Wao wanalala usingizi wakilipiwa mpaka kijiti ya meno.

Mimi hawa nawaona kama ni adui wakubwa na maisha yetu. Sifa kubwa na adui kufurahi kukuona ukiteseka
 
Back
Top Bottom