Wanauchumi na watu wa Fedha, nini sababu ya hili hapa?

The hammer

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
2,397
Reaction score
1,786
Wanauchumi naombeni ufafanuzi wa hili jambo.

Kwanini fedha yetu ipo hivi ukilinganisha na nchi nyingine ambazo tunazizidi kwa kila kitu,natoa mifano michache kwa kulinganisha thamani ya fedha za nchi mbalimbali kwa dollar ya Kimarekani.

1U.S $=2181.20 Tsh
1U.S $=640 Somali Shillings
1U.S $=556.50 Malawi Kwach
1U.S $=85.40Liberian Dollar
1U.S $=10.4p=Botswana Pula
1U.S $=13.62 Lesotho lot
1U.S $=446.05 Comoros Franc
1U.S $=21.11 ETB=Ethiopian Birr
1U.S $=38.60 Gambian Dalasi
1U.S $=1560.50Fbu=Burundi Franc
1U.S $=928.00 Congo Franc
1U.S $=8.03 Egyptian Pound
1U.S $=101.51Ksh
1U.S $=744.00RF=Rwanda Franc
1U.S $=3.81 Ghananian cedi
1U.S $=1.38 Libyan Dinar
1U.S $=326.50 Maurtania Ougulya
1U.S $=35.70 Mauritius Rupee
1U.S $=42.83 MT=Mozambique Metical
1U.S $=13.62 Namibian Dollar
1U.S $=198.95Nigerian Naira
1U.S $=13.56 South African Rand

Hivi hizi nchi zimefanyaje hadi fedha zao ziwe na thamani kubwa sana kuliko ya Tanzania?Wametuzidi kitu gani zaidi hadi Somalia
 
thamani ya fedha inawesa ikawa chini sana lakini uchumi wa nchi husika ukawa juu sana...
ni.mipango tu, tusililie sana thamani ya TZS ipate.
 
thamani ya fedha inawesa ikawa chini sana lakini uchumi wa nchi husika ukawa juu sana...
ni.mipango tu, tusililie sana thamani ya TZS ipate.

Hahaha unamanisha uchumi wa Tanzania ni mkubwa
 
inaweza ikasababishwa na uingizaji wa bidhaa bila kuwa na uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi,
Tanzania inauza bidhaa chache mno pamoja na malighafi huku ikipokea bidhaa nyingi mno kutoka nje hii inashusha thamani ya fedha.
 
Ndio maana nikatoa baadhi ya nchi ambazo tumezizid kwa kila kitu lakini wao fedha yao ipo juu sana kuliko ya kwetu,nchi kama Somalia,Malawi,Comoro sidhani kama wametuzidi kwenye export labda uje na majibu mengine
 
1$ = 22,325 Vietnamese Dong

Unaelezea vipi hapo?
 
thamani ya fedha inawesa ikawa chini sana lakini uchumi wa nchi husika ukawa juu sana...
ni.mipango tu, tusililie sana thamani ya TZS ipate.

Kumbe haina maana sana pesa kuwa na thamani hongera sana msomi wa Tz
 
inaweza ikasababishwa na uingizaji wa bidhaa bila kuwa na uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi,
Tanzania inauza bidhaa chache mno pamoja na malighafi huku ikipokea bidhaa nyingi mno kutoka nje hii inashusha thamani ya fedha.

Kumbe somalia bidhaa zao zinatoka sana kuzidi sisi aibu sana hii
 
Ndio maana nikatoa baadhi ya nchi ambazo tumezizid kwa kila kitu lakini wao fedha yao ipo juu sana kuliko ya kwetu,nchi kama Somalia,Malawi,Comoro sidhani kama wametuzidi kwenye export labda uje na majibu mengine

Nimekupenda sana kwa leo jinsi unavyo wapasua vichwa wachumi wa Tz
 
Exchange rate inatokana na demand/supply ya currency. Demand ikiongezeka thamani ya pesa inapanda demand ikishuka thamani inapungua.
Sasa demand/supply ya currency inategemea na vitu vingi ikiwemo inflation/mfumuko wa bei, interest rates/riba za kwenye mabenki, balance of payments/tofauti kati ya vitu unavyonunua kutoka nje na unavyouza nje, madeni ya serikali, economic stability ya nchi etc.

Kuwa na weak currency haimaanishi kuwa nchi yako ni maskini kama watu wengi wanavyodhani na nchi nyingi zinachukuaga hatua za makusudi kushusha thamani ya currency yao kama kuongeza hela zilizo kwenye mzunguko, hii husaidia exports kuongezeka.

Cheki Balance Of Payments (BOP) Definition | Investopedia
 
Value ya currency ikiwa chini sio faida kwa nchi inayoexport far much more than inaimport.
Ndio maana China wanashusha dhamani ya hela yao on purpose. They manufacture and export alot.
Sisi tuna nini cha kuexport?
 
Kumbe haina maana sana pesa kuwa na thamani hongera sana msomi wa Tz

sijasema haina maana ...ila kuna namna ya kuinua uchumi huku thamani ya pesa ikiwa chini, na kuna namna ya kuinua uchumi huku thamani ya pesa ikiwa juu.
 
Wasomi wa TZ bwana......
Value ya currency ikiwa chini sio faida kwa nchi inayoexport far much more than inaimport.
Ndio maana China wanashusha dhamani ya hela yao on purpose. They manufacture and export alot.
Sisi tuna nini cha kuexport?
Comprehension zero! Ndo nilichosema wanashusha thamani ya hela yao ili kusaidia exports. Sijasema kuwa TZ inaisaidia ila kuna nchi zinafanya.
 
Hahaha unamanisha uchumi wa Tanzania ni mkubwa

hujanielewa... hebu fuatilia China, wao wanashusha thamani ya Yuan dhidi ya Dollar purposely, hata sisi tukiwekeza kwenye viwanda na ku-export bidhaa tutafurahia TZS kushuka
 
Comprehension zero! Ndo nilichosema wanashusha thamani ya hela yao ili kusaidia exports. Sijasema kuwa TZ inaisaidia ila kuna nchi zinafanya.
Aliyeuliza swali ameuliza kwa context yetu sisi hapa Tanzania, wewe unaanza kumwambia eti kuwa na weak currency sio necessarily kitu kibaya.
 
hujanielewa... hebu fuatilia China, wao wanashusha thamani ya Yuan dhidi ya Dollar purposely, hata sisi tukiwekeza kwenye viwanda na ku-export bidhaa tutafurahia TZS kushuka

Unapotaja mifano usiweke nchi zilizoendelea,taja mifano kama Ethiopia,Kenya,Burundi n.k... swali ni kuwa kwanini currency zao ina thamani sana Kuliko Tsh?
 
1$ = 22,325 Vietnamese Dong

Unaelezea vipi hapo?

Nadhani pia Uchumi wa Vietenam ni mkubwa sana kuliko wa kwetu na kuna nchi nyingi thamani ya fedha yao ni ndogo lakini nimeangalia na uwezo wa uchumi wao na rasilimali zao.Ukinijibu kwanini thamani ya fedha ya Tanzania ni ndogo kuliko ya Burundi au Comoro nitafurahi zaidi.
 
Comprehension zero! Ndo nilichosema wanashusha thamani ya hela yao ili kusaidia exports. Sijasema kuwa TZ inaisaidia ila kuna nchi zinafanya.

Nimekuelewa vyema,sasa niambie kwanini thamani ya Tsh ipo chini sana ukilinganisha na ile ya Malawi au Comoro,I'll thank kama utatumia mifano ya nchi niliyoitoa hapo juu na sio zile zilizoendelea zaidi yetu kama nchi za Asia au Arab coutries
 
Hujui walichotuzidi? Walikubali kufanya mabadiliko.
Na mmewarudisha mtazidi kishangaa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…