Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mimi nishakaa maisha yote, kutoka home ushuani Obay mpaka nilipotoka nikaamua kujichanganya maisha ya Uswahilini Tabata Ubaya Ubaya - ya enzi hiyo, si ya leo. Huko kinamama wazaramo wazaramo tele, ukiwa unatoka asubuhi soap soap kwenda mjini, unarudi jioni huna story na mtu, wewe tayari deal. Ukiwa na uwezo wa kwenda bar kununua Safari mbili na chips mayai regularly wewe tayariunaonekana kibosile, watu wanauliza kwa nini hujaoa?Hahahah hujakutana na kina Chausiku wewe? MATAPELI WA KIWANGO CHA JUU
Maisha ya kina Sikudhani nyumba ya vyumba sita watoto wa uswahilini kukugongea mlango na kukuambia "mama kasema mkopeshe shilingi mia moja" nishaishi.
Na watoto wa kishua kina Danielle wa The Hamptons wanaopishana na Paris Hilton kwenye summer vacations zao Long Island nao nishakaa nao.
Ndiyo maana nakwambia stories zote nishazijua. Nikitaka kusaidia nitasaidia tu, lakini si kwa minajili ya kuwindana kwa hela za nauli.
It is petty and smallminded.