Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Kwenye suala la kubeba mimba mwenye maamuzi ni mwanamke
Kwa hiyo kisa kubeba mimba ni suala la mwanamke ndio mnaenda tu mkiwa mmefumba macho? Hapa inatuhusu wote ke kwa me, msiotaka kuzaa kwa muda huo tumieni kinga.

Suala la kuzaa si la kumuachia mwanamke pekee kuna wanawake wengine hawajielewi, akili mbovu kama mnavyodai wenyewe utaskia nilitegeshewa mimba sasa ili kuepuka yote hayo vaeni kinga, kuweni na huruma na damu zenu.
 
Ila watu hubadilika mkuu,
 
Mimi naona suluishi ni mwanaume kuwa makini tu na mtu wa kuzaa naye,kama imetokea umepata mtoto na mwanamke hakuna kumuacha upambane naye mlee mtoto/ watoto wenu,hakuna haja ya kutesa watoto ambao hawana mskosa kwa starehe zenu,period
 
Ni mtazamo nauheshimu
 
Huu ni ukweli ndugu,tatizo watu wanafanya maamuzi pasipo kuwaza matokeo yake,mama anamkimbua baba au baba anamkimbia mama ili kumkomoa bila kufikiria kuwa wanaoathirika ni watoto kwa kupata malezi ya upande mmoja tu,Mungu atusaidie
 
Kila mtu ana wakufanana Naye kunawatu huwa wanapinga ndoa kisa tu sio kabila moja
Hiyo sio sababu ya msingi. Kuna sababu za msingi na sababu holela au binafsi. Hatuwezi tumia sababu binafsi kujenga hoja za kijamii.

Mtu kama Giggy money anapopata mtoto na hana character nzuri kwanza tunakuwa tunaweka rehani ustawi wa jamii yetu sababu unategemea giggy anaweza lea mtoto kimaadili hadi akawa mtu mzima wa kulubalika na wastaarabu wengine kwenye jamii au ndio kuandaa mbegu za jeshi jipya la wadangaji hapa mjini?
 
Inaweza kuwa ajali mbona

Mara moja imo
Sasa muhimu ni sisi wanaume kuchukua hatua na kukaa mbali na mabinti au wanawake ambao hatutaweza kuishi nao na kulea nao watoto endapo mazingira hayataruhusu.

Kitendo cha Mwanaume kulala tu na mwanamke ambaye hautamudu kumuweka ndani kuishi nae tayari ni kosa na jinai ya kijamii sababu unashiriki jambo ambalo hautaweza kuishi na matokeo yake.
 
Umenena vyema mkuu
 
Na huku naomba MUNGU tusifike maana kwa akili za vijana wa bongo mimba zitatolewa sana jambo ambalo ni laana zingine kwa taifa.

Tujikite tu kwenye responsible manhood itatosha. Date na wanawake ambao unaweza kuwaweka ndani. Kama huwezi m'moja wapo wanawake hawanashida kuolewa kwa mume m'moja hata wakiwa 10 mradi tu uweze kuwapa upendo na care.

Shida ni hii tabia ya chovya kojoa kwenye kila shimo linalotamanisha.
 
We jamaa ni noma huu nimsumari wa moto na suluhu nikubadirika nikweli kabisa ukisemacho ila wadada wengine wanategesha mimba bila makubaliano mkuu.unakuta umemueleza ukweli kua hatuna mpango wakuzaa ila yy anakomaa tu.
Kimsingi hata kama ukikubaliana nae mwanamke huongea kwa akili A na kutenda kwa akili B. Maana yake usimuamini mwanamke kwa maneno yake ila matendo yake.

Kama amekukubalia kuwa hamtazaa utaona anagoma kufanya mapenzi na wewe nyakati fulani au hatakubali bila condoms but ukiona mnakubaliana ila anakuachia umpelekee moto kila unapojiskia jua nafsini mwake amesema wewe weka tu si utalea mtoto kwan taabu ipo wapi.

Hapa ndipo wanaume tunawajibika kujitathimini kwa maamuzi yetu. Kulala na mwanamke ukikubaliana nae kuwa msizae haitoshi kuwa makini na mbegu zako usitupe tupe hovyo kwasababu zinayoka kama risasi.

Askari mwenye akili hafyatui fyatui hovyo risasi zake kwasababu zipo nyingi anakuwa makini na anacholenga ili awe na shabaha ya kumfikia adui.
 
Ikitokea umepata mwanamke wa hovyo then still tuna nafasi ya kuwajibika kiume kwa kuchukua mtoto na kulea chini ya uangalizi wetu ili akue katika mazingira mazuri na rafiki.
 
Hapo sawa mwanamke akiwa mwendawazim hutakiwi kuzaa nae utajuta maisha yako yote
My point exactly. Majuto ya kuzaa na mwendawazimu au mwanamke asiyejitambua ni ya maisha yote. Utakuwa kila ukiwaona watoto unatamani ungewapa mama wa kueleweka ili waweze kuwa katika mazingira ya upendo na amani. Ila ndio umeshabugi na hauwezi rudisha muda nyuma.

Unaona mfano yule kijana aliyezaa na Giggy money kwan hakuwa akiona matukio na fujo za Giggy money?

Ila kwa upuuzi tu akajiona yeye ana akili kushinda nature akaacha kufuga kuku wa nyama atakata kufuga kunguru sijui ili iwe nini mwisho wa siku maana kunguru mbali na kwamba hafugiki lakini pia hana faida yoyote kusema utamla nyama kama kuku.

Leo mwanamke yule yule ambaye alipuuza kumuepuka anampelekesha mitandaoni na kumchafulia jina lake na familia yake hata pasipo kumchokoza au kumfanya lolote anashangaa anapigiwa simu "Wewe baba fulani umeona alichopost giggy leo huko Instagram, amekutukana balaa, kwan umefanyaje hadi kakasirika vile" kumbe Giggy money amekunywa tu savannah nyingi amevuta na bange zimeamsha wazimu akatafuta sababu ya kutoa kichaa chake na akaamua kumuwashia moto mwanaume aliyezaa nae mtoto.

Wewe unadhani yule kijana anajiskiaje kwasasa kuona mtoto wake analelewa na mama kama Giggy money ambaye anatumia pesa za udangaji kumtunza mtoto huku yeye akikosa access ya kukaa na mtoto lakini pia akitazama mtoto wake anakuwa katika mazingira ya fujo hivyo anajiskiaje? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Huyo still hatofaa sababu hatabakia. So kama imetokea amekengeuka baada ya kuwa pamoja then hauna budi ila kulea mwanao, why usichukue mtoto ulee kwa msaada wa mama yako na House girl? [emoji848]

Lkn hapa tulikuwa tunatetea haki ya mtoto awe na mama pamoja na baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…