Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Kwenye suala la kubeba mimba mwenye maamuzi ni mwanamke
Kwa hiyo kisa kubeba mimba ni suala la mwanamke ndio mnaenda tu mkiwa mmefumba macho? Hapa inatuhusu wote ke kwa me, msiotaka kuzaa kwa muda huo tumieni kinga.

Suala la kuzaa si la kumuachia mwanamke pekee kuna wanawake wengine hawajielewi, akili mbovu kama mnavyodai wenyewe utaskia nilitegeshewa mimba sasa ili kuepuka yote hayo vaeni kinga, kuweni na huruma na damu zenu.
 
1. Hapa sijaongelea wanaume kwa kuwalinganisha na wanawake bali nimeongea na sisi wanaume specifically bila kuwahusisha wanawake maana kila siku mbona huwa tunawapa makavu hapa. Ila kuna upande wa wanaume pia ambao wanatia hawa wanawake irresponsible why sasa umkojolee ndani na unajua anaweza beba mimba?

Kwann usibebeshe ujauzito mtu ambaye una uhakika huyu hata akibeba mtoto wangu nitaweza kuishi nae hata kama ilikuwa ni ajali. Unazaa na mtu hadi wazazi wako wanajiuliza walikosea wapi kwenye malezi yao hadi uwaletee kituko kama huyo mwanamke wako?

2. Wanawake tukubaliane tu hawana uwezo wa kujisimamia na upuuzi wao tunauona kwenye maamuzi yao kila siku. Sasa why tunawachagulia watoto wetu sampuli za hovyo za mama. Unaona kabisa huyu demu ni kilaza ila sababu mtamu unamkamulia tui la nazi, hivi haujisikii hata huzuni mtoto wako atakapokuja na akute huyo ndie mama uliyemuwekea? [emoji848]

Hapa sijawaona wanawake kama wajinga bali nimeavoid kuwaongelea kwenye uzi ili tufocus sisi wanaume tuambizane.
Ila watu hubadilika mkuu,
 
Mimi naona suluishi ni mwanaume kuwa makini tu na mtu wa kuzaa naye,kama imetokea umepata mtoto na mwanamke hakuna kumuacha upambane naye mlee mtoto/ watoto wenu,hakuna haja ya kutesa watoto ambao hawana mskosa kwa starehe zenu,period
 
Kwa hiyo kisa kubeba mimba ni suala la mwanamke ndio mnaenda tu mkiwa mmefumba macho? Hapa inatuhusu wote ke kwa me, msiotaka kuzaa kwa muda huo tumieni kinga.

Suala la kuzaa si la kumuachia mwanamke pekee kuna wanawake wengine hawajielewi, akili mbovu kama mnavyodai wenyewe utaskia nilitegeshewa mimba sasa ili kuepuka yote hayo vaeni kinga, kuweni na huruma na damu zenu.
Ni mtazamo nauheshimu
 
Jamii inaenda kufeli sana hii mzee. Watoto wanateseka sana mimi napataga huzuni sana kuona watoto wanakuzwa katika kizazi cha sasa ambacho baba na mama kuishi pamoja imekuwa ni nadra watoto wanaishi kwa hisia mpasuko sana.

Ipo siku nakwambia tutakuja kuyajutia haya matendo
Huu ni ukweli ndugu,tatizo watu wanafanya maamuzi pasipo kuwaza matokeo yake,mama anamkimbua baba au baba anamkimbia mama ili kumkomoa bila kufikiria kuwa wanaoathirika ni watoto kwa kupata malezi ya upande mmoja tu,Mungu atusaidie
 
Kila mtu ana wakufanana Naye kunawatu huwa wanapinga ndoa kisa tu sio kabila moja
Hiyo sio sababu ya msingi. Kuna sababu za msingi na sababu holela au binafsi. Hatuwezi tumia sababu binafsi kujenga hoja za kijamii.

Mtu kama Giggy money anapopata mtoto na hana character nzuri kwanza tunakuwa tunaweka rehani ustawi wa jamii yetu sababu unategemea giggy anaweza lea mtoto kimaadili hadi akawa mtu mzima wa kulubalika na wastaarabu wengine kwenye jamii au ndio kuandaa mbegu za jeshi jipya la wadangaji hapa mjini?
 
Inaweza kuwa ajali mbona

Mara moja imo
Sasa muhimu ni sisi wanaume kuchukua hatua na kukaa mbali na mabinti au wanawake ambao hatutaweza kuishi nao na kulea nao watoto endapo mazingira hayataruhusu.

Kitendo cha Mwanaume kulala tu na mwanamke ambaye hautamudu kumuweka ndani kuishi nae tayari ni kosa na jinai ya kijamii sababu unashiriki jambo ambalo hautaweza kuishi na matokeo yake.
 
Inakwaza na kufedhesha sana kwasasa kuona kuna ongezeko kubwa la watoto ambao hawajulikani baba zao ni akina nani na hata kama baba wanajulikana basi hawapo katika maisha ya mtoto.

Big up kwa akina baba ambao wanapambania kuwatunza na kuwalea watoto wao wa damu na kuwajibika kama baba na kutowatenga hawa watoto.

Kimsingi baba ni mtu muhimu sana katika maisha ya mtoto na baba anapokosekana katika maisha ya mtoto ni rahisi sana kwa mtoto kupoteza direction ya Maisha utu uzimani.

Mtoto wa kiume unakutana na mdada haujui history yake haumfahamu anaishi kwa mwenendo gani kisa tu kakuruhusu kumpelekea moto unaachia mbegu zako kwenye mji wake wa uzazi ukijua wazi matokeo yake ni yapi.

Hivi huwazii mtoto wako anapozaliwa huyo ndie atakuwa mama yake na wewe ndie baba yake na ndio mwanzo wa familia? Why sasa unaanzisha kitu kikubwa namna hiyo katika hali ya kizembe sana.

Hauoni kuwa unakuja kumpa maisha ya mateso na maumivu huyo mtoto ambaye alitakiwa kukuzwa kwenye maisha ya upendo wa baba na mama na yeye aje kuwa raia mwema?

Je, umemuwazia huyo mwanamke namna atateseka na mtoto huyo usiku pekee yake mchana pekee yake, hapo inakupa fahari gani kama mwanaume kuona damu yako ipo huko na wewe upo huku usijali inaishi maisha ya namna gani?

Kama kwako ni muhimu kuchuja nafaka, si upige hata nyeto au uzingatie ngono salama ambayo haitaleta mtoto ambaye hautakuwa hiyari kumlea kwa upendo?

Hivi unatakiwa uwe na akili ya namna gani hadi kukimbia mtoto wako mwenyewe ambaye hata ukimtazama unajiona kabisa wewe yule pale katika mwili na damu?

Hebu ifike muda tuanze kuambiana ukweli, hawa watoto tunaweza wapata katika mazingira salama na tukawalea. Kama mwanamke ni mkorofi hushindwi kuchukua mtoto wako ukapeleka kwa bibi yake yaani mama yako au ukatafuta mwanamke akusaidie kulea hata beki tatu wapo kibao ambao utamuacha pale room kwako akae na mtoto na wewe umpatie mshahara na akusaidie kuishi na mtoto wako vizuri tu hadi atakapofika umri wa kuanza kujisimamia.

Trust me, mtoto yupo salama zaidi akikua mazingira ya shida pembeni ya baba yake kulikoni akiishi maisha ya shida pembeni ya mama yake ambapo ni rahisi kuharibika tabia na kuwa tatizo ukubwani.

Siku zote linapokuja swala la kulea mtoto huwa wanaume kuna ile tabia ya kujitisha kuwa mtoto atateseka akilelewa na watu baki, huu ni upotoshaji mkubwa sana. Ipo mifano hai ya wanaume waliolea watoto wao wenyewe bila mama wa mtoto kwa msaada wa mfanyakazi na familia yake hadi mtoto kawa mtu mzima, si watoto wa kiume tu hata wa kike.

Inawezekana na nirahisi sana zaidi ya unavyofikiria. Mimi nimeshalea wajomba wawili kwa msaada wa bibi yao na dada wa kazi baada ya kuona upumbavu wa mama zao unavyowagharimu watoto. Ndio maana nauchukia sana usingle mother sababu naelewa madhara na mateso yake kwa watoto wasio na hatia.

Inaanza na wewe kuwajibika na sio kuwategemea hawa mabinti wa sasa ambao hawawajibiki na maamuzi yao. Kama wewe hautatoa mbegu zako kwa mtu ambaye hautaanza nae familia masingle mother watatokea wapi na watoto watapatikana vipi?

Hebu wanaume tuchague kuwajibika na sio kuwa vilaza ambao kwa makusudi tunachagua kushirikiana na wanawake irresponsible kuleta watoto duniani na kuwatesa bila hatia. Hebu tuanze kuwa na maono ya wapi tunapeleka uzao wetu ili tusipoteze mbegu zetu zikaotea mibani.

Utafurahi siku unakutana na binti yako amekuwa mdangaji, kahaba, ana ma'tattoo amekuwa mtu wa hovyo kama akina Giggy money, au Amber Rutty?

Au unakutana na mtoto wako wa kiume amekuwa kituko, kasuka marasta au kaweka dreads, matattoo mwili mzima, kavaa mlegezo, anakimbiza bodaboda halafu wewe ni mtu na heshima zako unapita, unaweza kumrekebisha tena samaki aliyekauka? Ni kazi rahisi sana kujenga kizazi bora kupitia malezi bora ya watoto kuliko kurekebisha taifa na jamii iliyoharibika kwa gharama na program za kuwarekebisha watu wazima ambao wamekomaa kiakili na wameshapinda.

Acheni kuzaa watoto ambao hamna mpango wa kuwalea na kuwatunza kwa upendo kifamilia mnatutesea watoto wasio na hatia na kuleta laana ambazo hazikuwa na nafasi kwenye jamii yetu. Watoto waliopo kwa sasa iwe ni funzo tubadilike.
Umenena vyema mkuu
 
Ndo excuses zenyewe hizo,kama haeleweki mbona akaenda mbali hadi wakashare mazito?
Sheria ndio itakuwa msumeno wa hiyo nonsense uwe umeoa ama la shughulika na salary inakatwa juu kwa juu before upokee ,mtoto apate matunzo,mbona wangetii.
Shida sasa mifumo yetu halijojo.
Na huku naomba MUNGU tusifike maana kwa akili za vijana wa bongo mimba zitatolewa sana jambo ambalo ni laana zingine kwa taifa.

Tujikite tu kwenye responsible manhood itatosha. Date na wanawake ambao unaweza kuwaweka ndani. Kama huwezi m'moja wapo wanawake hawanashida kuolewa kwa mume m'moja hata wakiwa 10 mradi tu uweze kuwapa upendo na care.

Shida ni hii tabia ya chovya kojoa kwenye kila shimo linalotamanisha.
 
We jamaa ni noma huu nimsumari wa moto na suluhu nikubadirika nikweli kabisa ukisemacho ila wadada wengine wanategesha mimba bila makubaliano mkuu.unakuta umemueleza ukweli kua hatuna mpango wakuzaa ila yy anakomaa tu.
Kimsingi hata kama ukikubaliana nae mwanamke huongea kwa akili A na kutenda kwa akili B. Maana yake usimuamini mwanamke kwa maneno yake ila matendo yake.

Kama amekukubalia kuwa hamtazaa utaona anagoma kufanya mapenzi na wewe nyakati fulani au hatakubali bila condoms but ukiona mnakubaliana ila anakuachia umpelekee moto kila unapojiskia jua nafsini mwake amesema wewe weka tu si utalea mtoto kwan taabu ipo wapi.

Hapa ndipo wanaume tunawajibika kujitathimini kwa maamuzi yetu. Kulala na mwanamke ukikubaliana nae kuwa msizae haitoshi kuwa makini na mbegu zako usitupe tupe hovyo kwasababu zinayoka kama risasi.

Askari mwenye akili hafyatui fyatui hovyo risasi zake kwasababu zipo nyingi anakuwa makini na anacholenga ili awe na shabaha ya kumfikia adui.
 
@Zemanda well said mkuu point taken wanaume tunapaswa kua makini nawanawake tunaodate nao maana ndio watakua mama wa watoto wetu.care killed the cat,mda mwingine maisha ndivyo yalivyo tu mkuu hawa wanawake waweza chunguza sana ila ukakutana nagumegume ndio ukazaa nalo.
Ikitokea umepata mwanamke wa hovyo then still tuna nafasi ya kuwajibika kiume kwa kuchukua mtoto na kulea chini ya uangalizi wetu ili akue katika mazingira mazuri na rafiki.
 
Hapo sawa mwanamke akiwa mwendawazim hutakiwi kuzaa nae utajuta maisha yako yote
My point exactly. Majuto ya kuzaa na mwendawazimu au mwanamke asiyejitambua ni ya maisha yote. Utakuwa kila ukiwaona watoto unatamani ungewapa mama wa kueleweka ili waweze kuwa katika mazingira ya upendo na amani. Ila ndio umeshabugi na hauwezi rudisha muda nyuma.

Unaona mfano yule kijana aliyezaa na Giggy money kwan hakuwa akiona matukio na fujo za Giggy money?

Ila kwa upuuzi tu akajiona yeye ana akili kushinda nature akaacha kufuga kuku wa nyama atakata kufuga kunguru sijui ili iwe nini mwisho wa siku maana kunguru mbali na kwamba hafugiki lakini pia hana faida yoyote kusema utamla nyama kama kuku.

Leo mwanamke yule yule ambaye alipuuza kumuepuka anampelekesha mitandaoni na kumchafulia jina lake na familia yake hata pasipo kumchokoza au kumfanya lolote anashangaa anapigiwa simu "Wewe baba fulani umeona alichopost giggy leo huko Instagram, amekutukana balaa, kwan umefanyaje hadi kakasirika vile" kumbe Giggy money amekunywa tu savannah nyingi amevuta na bange zimeamsha wazimu akatafuta sababu ya kutoa kichaa chake na akaamua kumuwashia moto mwanaume aliyezaa nae mtoto.

Wewe unadhani yule kijana anajiskiaje kwasasa kuona mtoto wake analelewa na mama kama Giggy money ambaye anatumia pesa za udangaji kumtunza mtoto huku yeye akikosa access ya kukaa na mtoto lakini pia akitazama mtoto wake anakuwa katika mazingira ya fujo hivyo anajiskiaje? [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Huyo still hatofaa sababu hatabakia. So kama imetokea amekengeuka baada ya kuwa pamoja then hauna budi ila kulea mwanao, why usichukue mtoto ulee kwa msaada wa mama yako na House girl? [emoji848]

Lkn hapa tulikuwa tunatetea haki ya mtoto awe na mama pamoja na baba
 
Back
Top Bottom