Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Hakuna mimba ya bahati mbaya isipokuwa ya kubakwa, au kwa minor, minor anaweza asielewe mzunguko vizuri au asielewe njia za uzazi wa mpango.

Binafsi ningemuomba metal mada aandike uzi wenye heading vise versa na hiyo ya sasa.
Ntalifanyia kazi hilo kwasababu naona wadada wanahisi wao hawana hatia.
 
Dogo punguza utahira basi kidogo, unavyowatetea wanawake mwisho wa siku unaonekana tahira hata kwa hao wanawake wenyewe....

Kwamba mwanaume ndio anachangia kwa 70% kwenye suala zima la mwanamke kubeba mimba? Dogo hivi ina umri gani kwanza?

Mwanamke kama hakuelewi au hajaipenda mbegu yako hawezi akakubebea mimba ng'ooo yaani hata umtombee vipi, kama hajapanga kuzaa na wewe huwezi kumpa mimba hata iweje kwenye zama hizi ambazo kuna njia chungu nzima za kuzuia mimba pamoja na cheap abortions.

Yaani kabisa umekaa hapa unakaza fuvu kwamba wanaume tuko responsible kwenye suala la ubebaji wa mimba, na wakati wao ndio waamuzi wa mwisho na akiamua asikuzalie hata kama mimba ina miezi sita anaweza akaipoteza na huna la kumfanya...

Wewe dogo unaonekana ni mgeni wa wanawake na tayari umeshamezwa na mfumo jike ambao umewafanya wanaume wengi wawe watetezi wa wanawake hata pale ambapo hakuna nmna sahihi ya kuwatetea.
True, very true mzee.
 
Mada nzuri changamoto za ujana ndio chanzo hadi unakuja kuzinduka unakuta ushampa mtoto wa watu mimba

Binafsi naona ni vyema kupambana na chanzo na si matokeo kwakuwa nyege siku zote hazina muongozo.

MAADILI ndio nguzo ya yote hayo, watoto wakike walelewe kama dhahabu wafichwe na wafunzwe kuona aibu na kukataa wanapotongozwa barabarani, wavikwe mavazi yenye stara toka wakiwa wadogo hadi wanakua, waamlishwe utiifu kwa wakubwa n.k

Vijana wakiume walelewe katika kujua nini maana ya uwanaume na si kushinda kutongoza visichana na tabia zingine za kihuni wakizani kuwa ndio uwanaume(uwanaume una miiko), wafunzwe heshima na kuwaheshimu wanawake sio kutukana mitusi ya nguoni barabarani kuwatukana wazazi wao wa kike ni upuuzi.

Na yote hayo yanaweza kufanyika kuanzia ngazi ya familia, ukoo, kijiji, mji mpaka taifa kwa ujumla mfano mzuri ni kijiji cha huko Arusha(nimeona fb) wameweka by-law na kukataza wadada kuvaa nusu uchi,mfano mwingine ni nchi za kiarabu zimefanikiwa kutunza maadili kwa kiasi fulani.
Very true. Shida familia za sasa zinachangamoto nyingi sana za kiustawi. Watu wanawaza sana pesa. Wanawake vichwa vipo speed sana na pesa ukimuuliza unachowahi hata hajielewi kama mwizi anaetaka kutoroka.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma binti akiwekwa mimba anafukuzwa nyumbani. Anaambiwa nenda kaishi kwa huyo aliyekupa mimba. Tena wababa ndiyo walikuwa wakali hivyo binti lazima aende kwa mwanaume aliyempatia mimba wataishi pamoja then mwanaume atafanya utaratibu wa kujitambulisha. Kwa sasa mabinti wengi wanalelewa na single mom hivyo hata akipata mimba hakuna wa kumlazimisha aende kwa mwanaume. Mwishoni naye anakuwa single mom. Pia nyumba aliyokuwa na baba ilikuwa inaogopeka hivyo hata vijana wa kiume walikuwa wanaogopa kwamba hapa nikiweka mimba Msala kwangu. Leo hii nyumba hazina mwanaume heshima uoga umepotea. Kizazi kinazidi kuharibika, vijana waliolelewa na single mom wengi wao hawana adabu, mabangi, matusi hovyo hovyo ni shida kwa kweli.
Familia ambayo haina baba wahuni huwa wanatembeza pesa tu hapo ndani hadi kinaeleweka. Kwanza bi wakubwa huwa wanakuwa wapole wakiona mwanaume yupo vema. Na kuna muda hawa wamama wanawafichia mabinti zao siri za wanaume hata sita kwa wakati m'moja mama anakuwa mshiriki wa kuficha uhaini wa binti yake kwenye tabia zake za hovyo.
 
Experience.kama mama ni sawa ataweza zuia ila sio kwa kila wakati kwa sababu maisha ni hayatabiriki so ni bora wote kutunzana na kutumia condom au mwanaume anywe vidonge vyakutompa mwanamke mimba hadi pale aoe nke amtakaye.
 
Inakwaza na kufedhesha sana kwasasa kuona kuna ongezeko kubwa la watoto ambao hawajulikani baba zao ni akina nani na hata kama baba wanajulikana basi hawapo katika maisha ya mtoto.

Big up kwa akina baba ambao wanapambania kuwatunza na kuwalea watoto wao wa damu na kuwajibika kama baba na kutowatenga hawa watoto.

Kimsingi baba ni mtu muhimu sana katika maisha ya mtoto na baba anapokosekana katika maisha ya mtoto ni rahisi sana kwa mtoto kupoteza direction ya Maisha utu uzimani.

Mtoto wa kiume unakutana na mdada haujui history yake haumfahamu anaishi kwa mwenendo gani kisa tu kakuruhusu kumpelekea moto unaachia mbegu zako kwenye mji wake wa uzazi ukijua wazi matokeo yake ni yapi.

Hivi huwazii mtoto wako anapozaliwa huyo ndie atakuwa mama yake na wewe ndie baba yake na ndio mwanzo wa familia? Why sasa unaanzisha kitu kikubwa namna hiyo katika hali ya kizembe sana.

Hauoni kuwa unakuja kumpa maisha ya mateso na maumivu huyo mtoto ambaye alitakiwa kukuzwa kwenye maisha ya upendo wa baba na mama na yeye aje kuwa raia mwema?

Je, umemuwazia huyo mwanamke namna atateseka na mtoto huyo usiku pekee yake mchana pekee yake, hapo inakupa fahari gani kama mwanaume kuona damu yako ipo huko na wewe upo huku usijali inaishi maisha ya namna gani?

Kama kwako ni muhimu kuchuja nafaka, si upige hata nyeto au uzingatie ngono salama ambayo haitaleta mtoto ambaye hautakuwa hiyari kumlea kwa upendo?

Hivi unatakiwa uwe na akili ya namna gani hadi kukimbia mtoto wako mwenyewe ambaye hata ukimtazama unajiona kabisa wewe yule pale katika mwili na damu?

Hebu ifike muda tuanze kuambiana ukweli, hawa watoto tunaweza wapata katika mazingira salama na tukawalea. Kama mwanamke ni mkorofi hushindwi kuchukua mtoto wako ukapeleka kwa bibi yake yaani mama yako au ukatafuta mwanamke akusaidie kulea hata beki tatu wapo kibao ambao utamuacha pale room kwako akae na mtoto na wewe umpatie mshahara na akusaidie kuishi na mtoto wako vizuri tu hadi atakapofika umri wa kuanza kujisimamia.

Trust me, mtoto yupo salama zaidi akikua mazingira ya shida pembeni ya baba yake kulikoni akiishi maisha ya shida pembeni ya mama yake ambapo ni rahisi kuharibika tabia na kuwa tatizo ukubwani.

Siku zote linapokuja swala la kulea mtoto huwa wanaume kuna ile tabia ya kujitisha kuwa mtoto atateseka akilelewa na watu baki, huu ni upotoshaji mkubwa sana. Ipo mifano hai ya wanaume waliolea watoto wao wenyewe bila mama wa mtoto kwa msaada wa mfanyakazi na familia yake hadi mtoto kawa mtu mzima, si watoto wa kiume tu hata wa kike.

Inawezekana na nirahisi sana zaidi ya unavyofikiria. Mimi nimeshalea wajomba wawili kwa msaada wa bibi yao na dada wa kazi baada ya kuona upumbavu wa mama zao unavyowagharimu watoto. Ndio maana nauchukia sana usingle mother sababu naelewa madhara na mateso yake kwa watoto wasio na hatia.

Inaanza na wewe kuwajibika na sio kuwategemea hawa mabinti wa sasa ambao hawawajibiki na maamuzi yao. Kama wewe hautatoa mbegu zako kwa mtu ambaye hautaanza nae familia masingle mother watatokea wapi na watoto watapatikana vipi?

Hebu wanaume tuchague kuwajibika na sio kuwa vilaza ambao kwa makusudi tunachagua kushirikiana na wanawake irresponsible kuleta watoto duniani na kuwatesa bila hatia. Hebu tuanze kuwa na maono ya wapi tunapeleka uzao wetu ili tusipoteze mbegu zetu zikaotea mibani.

Utafurahi siku unakutana na binti yako amekuwa mdangaji, kahaba, ana ma'tattoo amekuwa mtu wa hovyo kama akina Giggy money, au Amber Rutty?

Au unakutana na mtoto wako wa kiume amekuwa kituko, kasuka marasta au kaweka dreads, matattoo mwili mzima, kavaa mlegezo, anakimbiza bodaboda halafu wewe ni mtu na heshima zako unapita, unaweza kumrekebisha tena samaki aliyekauka? Ni kazi rahisi sana kujenga kizazi bora kupitia malezi bora ya watoto kuliko kurekebisha taifa na jamii iliyoharibika kwa gharama na program za kuwarekebisha watu wazima ambao wamekomaa kiakili na wameshapinda.

Acheni kuzaa watoto ambao hamna mpango wa kuwalea na kuwatunza kwa upendo kifamilia mnatutesea watoto wasio na hatia na kuleta laana ambazo hazikuwa na nafasi kwenye jamii yetu. Watoto waliopo kwa sasa iwe ni funzo tubadilike.
Kupata mimba ni uamuzi wa mwanamke.

Asipokupa utampaje mimba?

Wanawake waache kujirahisisha kwanza kwa wanaume ndipo hili suala litapungua au muhusika ataweza kujiepusha.

Mwanamke akisaidiwa kitu kidogo tu then anaanza kuwaza kulipa fadhila kwa kumbless, kwani fadhila ni kwa kumbless tu, hakuna fadhila za namna nyingine?

Kama ameamua kubless basi awe tayari na matokeo yake.

Hivi wewe unayemiliki shamba unampa mtu kwa utashi wako ili alime halafu baadae uanze kumlaumu? hiyo ni akili kweli?
 
Wanawake huwa wanatabia ya kuigiza.
U-single mother hutokea kwa namna nyingi unaweza kumuoa, ukapata mtoto halafu ukagundua mkeo anagongwa na jamaa huko nje.
Unapogundua kuwa mwanamke wako analeta mambo Meusi usipoteze muda ukachoma hisia zako ambazo unatakiwa kuzitumia kupenda wewe ukazitumia kuumia.

Mtoto wa kike akileta habari za makando chukua mtoto badilisha mlezi hata kama yeye yupo vizuri. Kitendo cha kuzingua baba wa mtoto tayari ni mwanzo wa kuzorotesha malezi maana atajenga mazingira ya mtoto kulelewa na baba mwingine so sidhani kama unataka hilo.

Mkishindwana beba mtoto wako aende anakopendwa akapate watoto wengine huko. Wewe chukua mtoto tafuta house girl au kama unabahati ya kupata mwanamke mpya akusaidie kulea mtoto wako unalea fresh tu bila shida hadi anafika umri wa kuongea nae na mkaelewana vema huko kuanzia miaka 6 kuendelea utaweza ishi nae hata wawili tu.
 
Hapa unakuta hujamdanganya ila baada tu ya kuzaa mkaishi kidogo mwanamke anabadilika apo unagundua ni bomu unachimba.
Unaondoka na mtoto wako mzee unaogopa kusepa na mtoto?

Point ya msingi ni kutoacha damu yako iteseke na unaweza kuitetea. Yule ni mtoto wako huwezi shindwa mpambania.
 
Paragraph yangu ya kwanza umeisoma? Omba sana kwenye maisha yako hata ukichepuka husikutane na mwanamke mlozi (sijui kama unaamini vitu kama hivi,ila vipo na watu wanafanyiwa hasa wanaume walio kwenye ndoa).
Yeah hiyo ipo sana. Ila jambo la msingi ni kuwa usalama tunajikadiria wenyewe.
 
Wapo wanakutegeshea wenyew...unamuuliza kabisa kama yupo kweny red line yeye anajibu hapana...Leo azae na ww
Usimuulize mwanamke kuhusu kalenda yake. Wewe jua kuchukua tahadhari kulinda uzao wako.

Kama umekutana nae tu hamuishi wote tumia kinga maana kuna magonjwa pia.

Kama ni mwanamke mnaonana mara kwa mara tayari utakuwa unajua cycle yake ya ovulation.

Nadhani ni umakini tu inahitajika. Usijiachie kama upo salama kihivyo.
 
Amezaa na bint wakazi wake rejea kichwa cha thread
Ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23] sijajua hiyo skendo mzee. Kumbe jamaa nae na principles zake zile anazingua huku ground?
 
Experience.kama mama ni sawa ataweza zuia ila sio kwa kila wakati kwa sababu maisha ni hayatabiriki so ni bora wote kutunzana na kutumia condom au mwanaume anywe vidonge vyakutompa mwanamke mimba hadi pale aoe nke amtakaye.
Kwann ulale na mtu ambaye hauna mpango wa kuoa halafu mnaigizia mnapendana. Kama vipi si unavuta kahaba unapiga inaisha.
 
Kupata mimba ni uamuzi wa mwanamke.

Asipokupa utampaje mimba?

Wanawake waache kujirahisisha kwanza kwa wanaume ndipo hili suala litapungua au muhusika ataweza kujiepusha.

Mwanamke akisaidiwa kitu kidogo tu then anaanza kuwaza kulipa fadhila kwa kumbless, kwani fadhila ni kwa kumbless tu, hakuna fadhila za namna nyingine?

Kama ameamua kubless basi awe tayari na matokeo yake.

Hivi wewe unayemiliki shamba unampa mtu kwa utashi wako ili alime halafu baadae uanze kumlaumu? hiyo ni akili kweli?
Mfano serikali wakabidhi mamlaka tra ya kufuatilia wanaume watoe matunzo ya mtoto kwa ulazima na ukishindwa utachezea makato kila kona kuanzia mshahara, ukitumiwa muamala, popote, ukiomba mkopo ukitoka tu unapigwa panga.

Halafu tuone kama itakuwa ni uamuzi wa mwanamke tu kubeba mimba. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nadhani kuna swala la kujitambua na kutoruhusu mbegu zako zisambae kama unamwaga takataka vile
 
Mfano serikali wakabidhi mamlaka tra ya kufuatilia wanaume watoe matunzo ya mtoto kwa ulazima na ukishindwa utachezea makato kila kona kuanzia mshahara, ukitumiwa muamala, popote, ukiomba mkopo ukitoka tu unapigwa panga.

Halafu tuone kama itakuwa ni uamuzi wa mwanamke tu kubeba mimba. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nadhani kuna swala la kujitambua na kutoruhusu mbegu zako zisambae kama unamwaga takataka vile
Hapo unataka upromote ngono sasa.

Mwanamke akijua atanufaika kwa namna hiyo mbona ataitafuta mimba kwa udi na uvumba.

Ukweli utabaki pale pale, suala la mimba ni uamuzi wa mwanamke.
 
Back
Top Bottom