Wanaume acheni ubabe kwenye kupima afya zenu

Wanaume acheni ubabe kwenye kupima afya zenu

Mchaga Tajiri

Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
10
Reaction score
16
Bado baadhi ya wanaume wanashindwa kupima afya zao wakitegemea majibu kutoka kwa wenza wao.

Hali hii imekuwa ikiwaumiza wanawake wengi hasa wanawake wajawazito bila ya kujua wafanye nini Ili kuwafanya wenzao wao wawe na muamko wa kupima afya zao.

"Nilipomuambia mume wangu inahitajika mimi na yeye kwenda kupima afya zetu aliniambia kwamba mimi nikiwa mzima na yeye atakuwa mzima," alisema mama huyo ambaye ni mjamzito.

Mara kadhaa wanaume wamekuwa wakihimizwa kuchunguza afya zao lakini wamekuwa na muako mdogo, wengi wao wakiwa na kisingizio cha kwamba wako na majukumu mengi ya kazi na kadhalika.

1682002846894.jpeg

Picha kutoka maktaba
 
Back
Top Bottom