Wanaume hatukubali kushindwa kwenye Mapenzi!!! Wanawake je?

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Ni kitu ambacho nimesha-experience, lakini interaction na wanaume wenzangu nimagundua kuwa wengi tupo hivyo...

Wanaume hawapendi kuachwa na mwanamke. Hata kama mwanaume yupo na mwanamke na hampendi na anatafuta namna ya kumuacha, siku huyo mwanamke akamuwahi akampiga chini, mwanaume ataumia sana na tena kwa muda mrefu sana. Nimeshaona wanaume wanatumia nguvu nyingi sana kuwarudisha wanawake waliowaacha japo walikuwa hawawapendi. Mara nyingi hatusemi lakini huwa mwanaume anaumia sana anapoachwa, na mbaya zaidi agundue kuwa kaachwa baada ya mwanamke kupata mwanaume mwingine.

Najua hii ni natural behavior, kuwa mwanaume hapendi kuachwa, ka hata kama mapenzi yameshakufa na kuachana ndiyo next step, mwanaume atataka yeye ndiye atamke "Kuanzia leo, mimi na wewe tuachane (au kuanzia leo nimekuacha)".

Swali ninalouliza ni kuwa hivi kwa wanawake nao iko hivyo? Yaani mwanaume ambaye pengine mko pamoja lakini unahisi kabisa humpendi tena na unatamani muachane, hivi akikutamkia kuwa kakuacha unaumia?
 
usiombe ukutane na mwanamke wa hivyo
wakati npo shule nili mpiga kibuti msichana fulani...
amini usiamini alienda 'kunishtaki' kwa mama...lol
achilia mbali usumbufu mwingine na vitisho juu....

ngoja watu waje hapa wasimulie...
wanawake ndo zaidi .....
chunguza wanawake waliopewa talaka uone
utawahurumia wanavyo hangaika kwa waganga au kwenye maombi mume arudi...lol
 
Kama simpendi nashangilia na kupo shampeni.
Ebwanae uachwe pale ulipofika bei, hapo kimbembe kwa kweli.

Ila kama simpendi, wala !
 
Kuliko kuachwa, bora uache. Mara nyingi ukiona hali inabadilika unawahi wewe kupiga kibuti.

Mimi nilishapigwa kibuti ila jamaa (bila kuhangaika) akarudi mwenyewe; ila nilivyoona it won't work, nikampiga mimi kibuti, ndio nikapata amani.
 
Ukichwa na usiyempenda unamshukuru mungu maana anakusaidia ile process ya kumwambua sikutaki... Ila ka unampenda kweli inauma sanaaaaa
 
kuachwa kunauma ila kama mtu ulisha mchoka akikwambia tuachane unasema hewalaaaaaaaa.
 
Mimi demu kama simtaki akiniambia tuachane nashangilia sana, na wala hainiumi.
 
Nadhani inategemea pia unaachwaje. Kuna mtu hata kama mnataka kuachana lakini anakwambia yafuatayo:
- mwanaume / mwanamke gani wewe?
- huna lolote we bure kabisa?!?
- wakiitwa wanaume wewe utatoka?
- we mshamba tu huwezi lolote

Hayo ni machache tu ila yanakufanya ubaki na maswali mengi sana hata kama umeona mmefika ukingoni. Tutake tusitake, hakuna anayetaka kuachwa hata siku moja

Wanaume ego ndiyo inasumbua zaidi. Mtu akikupotezea na kakuambia maneno hayo hapo juu na may be umewahi kujishuku kwa hili au lile au hujiamini katika hili au lile basi mtu anaweza kukuchukia hadi siku anaingia kaburini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…