Wanaume Hawana Dogo. Wampachika Mimba Rapper Chemical na kumkimbia

Wanaume Hawana Dogo. Wampachika Mimba Rapper Chemical na kumkimbia

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Rapa wa kike nchini mwenye muonekano wa kiume Chemical akiongea na Times Fm amekiri kuwa ana mimba ya miezi saba ya mwanaume ambaye sio wa Dar ndio maana amekuwa kimya kimuziki na pia hapost picha mpya instagram.

Chemical amesema Mwanaume huyo aliyempa mimba amemkimbia ndio sababu kila siku amekuwa akisema atajioa kwa sababu ndiye mwanaume aliyekuwa anamtegemea kuwa angemuoa.

Chemical amesema kuolewa muda ukifika ni lazima. Lakini amesema yeye Hana time kabisa na mwanaume anayemjia na sound za kumbadilisha kimuonekano.

Chemical amesema anajikubali alivyo Hana muda wa kusubiri wa kumbadilisha ikitokea ni maamuzi yake Kama alivyoamua sasa.

Chemical ameongeza kuwa hapendi wanaume wenye miili ya wabeba vyuma wala wanaume wanene au wenye furushi la kitambi, yeye anataka mwanaume mwenye mwili simple tu wa kawaida
 
Back
Top Bottom