Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Siku moja nilikuwa nimekaa na vijana wenzangu tukipita pita mtandaoni, ndipo tukakutana na video ya dada mmoja akicheza.
Bila hata kufikiria sana, tukaanza kumshambulia kwenye comments. Mmoja akasema, “Huyu anacheza kama roboti.” Mwingine akaongeza maneno yake, na mimi nikajikuta naingia kwenye mstari wa kumchoma zaidi.
Ghafla, kaka yangu akaingia kwenye comments.
Nilidhani atacheka na sisi kama kawaida, kumbe ndiyo kwanza akaanza kutukemea.
Akatwambia, “Hivi mnaona hizi comments zenu ni kawaida? Huu ni ukatili wa mtandaoni. Kama hamna cha kujenga, si lazima kumshambulia mtu.”
Tukamcheka kidogo, lakini hakutulia.
Akaendelea kusema kwamba sisi wanaume tuna jukumu pia la kukemea na kutoa elimu pale tunapoona mwanamke anafanyiwa ukatili mtandaoni.
Sasa hapa ndipo nilipoanza kujiuliza...
Kaka yangu anaingilia mambo yasiyomhusu, au anafanya kitu ambacho wanaume wengi tunapaswa kufanya?
Kwa sababu ukweli ni kwamba, mara nyingi tunapoona mwanamke anashambuliwa mtandaoni, tunacheka, tunaongeza maneno au tunanyamaza.
Lakini huyu jamaa ameamua kusimama upande wa yule anayeshambuliwa.
Sasa sijui nimchane kwa kusema anaingilia “mambo ya kike,” au nimkubalie kwamba labda kuna mambo ambayo hayahitaji kuwa ya kike au ya kiume—yanahitaji tu utu.
Ninyi mnamuelewaje bro wangu? Anaizingua au yuko sahihi? Na kwa mwanaume, mnapaswa kufanya nini mkiona mwanamke anafanyiwa ukatili mtandaoni?