Wanaume: Jitihada zetu za kutafuta maisha Zinatuangamiza

Wanaume: Jitihada zetu za kutafuta maisha Zinatuangamiza

Kiokotee

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,675
Reaction score
2,211
Wanaume Tubadilike Tunatafuta maisha kwa nguvu zote kwa Ajili ya familia zetu na inapotokea tumefanikiwa tunafeli sehemu ndogo sana:
.Adui huwa hatoki mbali na wewe hata siku moja.
.Kwa nn watu waanze kukutafuta baada ya mafanikio.
.Kuna watu walikuwa hawana Time kabisa na wewe Utashangaa hata namba zako wametoa wapi?
.Hata ndugu waliokuwa hawakujali wataanza kukuona wa maana.
.Ndugu zako wengine unakuja kuwajua ukubwani tena baada ya mafanikio,Huenda kipindi Mzazi wako anakuhangaikia wao walikuwa wanakula maisha.
》》Usilipize Sio lazima kila mtu awe karibu na wewe na sio kila mtu analazimisha Ukaribu nawe ni mwema kwako,Mwingine anatafuta Data za kukuangamizia kwa hiyo lazima awe karibu yako akikosa atamtumia mtu yeyote wa karibu yako!!
N.B: Ninawindwa na watu wa karibu sana ambao hawajui nimeshawajua
Bila wenyewe kujua,Ila wanashangaa
Wananikosaje? Tuwe makini sana na Ndugu zetu jamani,ni watu hatari sana!
 
Pata pesa ndio ujue kuwa ndugu zako wachawi..

Pata pesa marafiki zako wa karibu wawe wanafki..

Pata pesa mtaani kwenu uanze kulogwa..

Pesa ni shetani kwa kweli

Baadhi ya Marafiki watakutenga .. amini

Baadhi ya ndugu zako watakulalamikia.. amini

Utakimbia mtaani kwenu na utatafuta pahala pa kuishi.. amini

Ila kwa ushauri mnaopataga pesa na ninyi badilini mind set zenu.. msipobadili au kuzijenga uzuri kila mtu mtamuona hafai siku unafilisika hauna hata rafiki..

Wapeni hata kidogo pesa wanaowapiga vizinga..

Tembeleeni ndugu/marafiki zenu wa zamani mliokuwa mnaangaika wote kutafuta maisha na kupeana moyo..

Hamjakatazwa kuwa bize na mambo/kazi zenu ila mnapopata nafasi jichanganyeni kwenye jamii zenu hata kwa udogo..

Mambo mengine mnayasababisha ninyi wenyewe.. mjitathimini basi mara nyingine hatuna shida na pesa zenu tunawamisigi kuwaona tu na kupiga story na ninyi kama zamani mlipokuwa hamna kitu.. pesa zenu zisitutenganishe .. hakuna atayezikwa na pesa zake wajameni..
 
Ukipata pesa ukaamua kuwapa ajira ndugu na jamaa zako Ili walegeze vyuma ikitokea tu ndugu kafa utaitwa freemason umemtoa kafara.
 
Back
Top Bottom