Wanaume kama umetelekeza mtoto kijijini nenda kamchukue

Wanaume kama umetelekeza mtoto kijijini nenda kamchukue

Wakuu wasalaam..

Niko vijiji vya ndani ndani huku Ndiwili wilaya ya kilolo nimekuja kwa shughuli zangu..baridi ni kali .

Katika matembezi yangu nikakutana na watoto wadogo chini ya miaka 10 wengi ni 7 na 8 wakifanya vibarua vya kusomba mbao yaani kuzitoa msituni na kuzipeleka lilipo gari ili tu wapate pesa ya madaftari na kwendea mnadani kununua nguo hasa "majaketi" ndo wanazungumzia sana.

Katika kuongea nao kuhusu wazazi, baadhi yao wanakaa na bibi na wengine na mama pia ila baba zao wanasikiaga wapo mjini.

Roho imeniuma sana , watoto wadogo lakini wamejivika majukumu ya kikubwa.

Mtoto kama huyu hawezi kuwa na huruma wala upendo kwa mtu baadae maana hajui neno huruma wala upendo.

Watoto hawa wanawakilisha maelfu ya watoto wengi walioko vijijini.

Wanaume kama umeacha mtoto huko vijijini eti yuko na mama yake sijui bibi yake fanya juu chini kamchukue uishi nae mwenyewe..

Kuna sehemu za nchi ukipita unaweza sema ndani ya Tanzania kuna nchi nyingine.
Wanaume ni watu wenye upendo sana ukiona mtoto anateseka basi ujue hata baba yake anateseka mara mbili hakuna Mwanaume anayekuwa financial stable akaacha damu yake.

Hao watoto utakuta baba zao wengi ni walevi, drug addict walio kata tamaa kujitunza wenyewe ni big issue sembuse kumchukua mtoto kijijini kuja naye mjini si ndio future ya mtoto inakuwa falling kabisa
 
Mwagito pede ndauli?

Hayo maisha ndio tumekulia sisi watu 2000 kurudi nyuma! Ndio maana unaona leo tuko ngangari,

Wewe unataka wakachukuliwe waje mjini wawe mashoga?
Ngoja wakomae hao wakifikisha miaka 18 wanatawanyika sehemu mbalimbali nchini na yanakuwa majembe hasa.

Yani unataka waje kurundikana huku mjini wawe madereva bodaboda?
Asante kalesa
 
Kwani hakuna familia zinazoanzishwa vijijini? Mpaka kusema watoto wengi waliopo huko wazazi wao wapo mijini
Mkuu zipo familia zinaanzishwa lakini changamoto za ngono zembe ni kubwa sana. Mabinti wadogo wanapata mimba alafu wazazi ndio hao boda boda au wanafunzi wenzao, wengine ni wale waliomaliza kidato cha nne au darasa la saba wanaokimbilia mijini,huko wanapata ujauzito na wanaume wasioeleweka au tabia zao za kuwa na msururu wa wanaume kwa lengo la kupata fedha au ndoa) hufanya mimba zao kukataliwa. Hao nao baada ya kujifungua hupeleka watoto vijijini.

Kingine ni Mila ya baadhi ya makabila hasa Kanda ya ziwa, Binti analazimika kuzaa Ili aache mtoto nyumbani, kwa kiLe kinachoitwa kuongeza ukoo.

Nimefanya project fulani vijijini na hilo nina ushuhuda nalo.
 
Back
Top Bottom