Wanaume kutumia avatar za kike

Wanaume kutumia avatar za kike

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
11,258
Reaction score
20,386
Ndugu wanabodi kuna hii hali ya baadhi ya wana JamiiForums kutumia avatar za kike ilihali ni wanaume imekaaje?

Kiuhalisia humu hatufahamiani kwa majina halisi ama sura halisi, mara nyingi wanadamu huwa tuna perceive vitu kulingana na kinavyoonekana na kuwa na assumptions fulani juu ya mtu ama kitu.

Mwanaume unapoweka avatar ya kike kama utambulisho wako ( haijalishi real or fake) inawafanya wengi wafikiri kuwa wewe ni wa jinsia ya -KE, hii si nzuri kwani unaweza kushangaa mwanaume mwenzio anaibuka PM kukuomba ama kukuhitaji.

Nini maoni yenu wanabodi?
 
Waweke tuu ilimradi hawavunji sheria!!!

Kwa wale wapenda pm watapambana tu na hali zao!!
 
sasa si unazipotezea tu, zinakusumbua nini huku hazikuhusu!
ila we ni mgumu kuelewa, sisemi kwamba zinaninyima usingizi bali naangalia namna ya social interaction ilivyo na jinsi saikolojia inavyotenga watu kulingana na gender perception
 
Mkuu bando lake..
Muda wa kufungua acc ni wake...
Avatar kaitafuta kwa muda wake..
Wewe unawashwa washwa na nini?
Hili ndio tatizo kuu la binadamu , kufwatilima mambo yasiyo ya muhimu na yasiyowahusu wakati umejaza chungu ya matatizo tena makubwa zaidi ya fake avatar
 
Ndugu wanabodi kuna hii hali ya baadhi ya wana JamiiForums kutumia avatar za kike ilihali ni wanaume imekaaje?

Kiuhalisia humu hatufahamiani kwa majina halisi ama sura halisi, mara nyingi wanadamu huwa tuna perceive vitu kulingana na kinavyoonekana na kuwa na assumptions fulani juu ya mtu ama kitu.

Mwanaume unapoweka avatar ya kike kama utambulisho wako ( haijalishi real or fake) inawafanya wengi wafikiri kuwa wewe ni wa jinsia ya -KE, hii si nzuri kwani unaweza kushangaa mwanaume mwenzio anaibuka PM kukuomba ama kukuhitaji.

Nini maoni yenu wanabodi?
mkuu hiki kitu kinafedhehesha sana na usipokuwa makini unaweza pata matatizo ya kisaikolojia, maana kitendo tu cha kupigwa sound na mwanaume mwenzako hata kama ni feki inatocha zake na huwa ni mwanzo wa hata kuwa shoga.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hahaha, na ndio kero yangu haswaaa, lakini kuna watu wanajibu mkato kama vile labda nimewaonea sana hao wenye hizo avatar
 
Mwanaume unapojitambulisha kwa avatar ya mwanamke ni hatari sana, na hili ni tatizo mbona wao wanawake hawaweki avatar za kiume? Halaf unakuta umeweka avatar ya mwanamke mwenye makalio Mkubwa amebinua
 
Sijawahi kuamini kama kweli kuna njemba za namna hii hapa JF.
Kama wapo, aisee, nimeamini hatufanani.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hahaha, na ndio kero yangu haswaaa, lakini kuna watu wanajibu mkato kama vile labda nimewaonea sana hao wenye hizo avatar
mimi kuna siku jamaa nadhani alipitiwa tu akanifikiria demu akawa ananipiga sound, hadi leo najisikia vibaya mno mtu kunihisi mwanamke.
 
Hahaaa... Mkuu
Mimi ni mmoja wapo ambao natumia avatar ya kike,

Sababu ni kwamba hakuna sheria inayosema mwanamke atumie avatar ya kike au ya kiume hata hivyo ukitaka kumfuata mtu pm angalia kwanza akaunti yake isome vyema kwa umakini wala usikurupuke.

Mimi nimepata meseji kama hizo za usumbufu kutoa kwa wanaume lakini huwa sijibu ila nafuta meseji na kuendelea na mambo mengine.

Tatizo watu hasa watz hukariri kuwa I'd ya kike ni mwanamke na I'd ya kiume ni mwanaume ikitokea I'd ya kike ni mwanaume basi hudhani ni shoga sasa kama amemuweka mwanamke lakini ni rafiki yake au ndugu yake au mchumba wake au mama yake au role model wake utajuaje acheni kuishi kwa kukariri,

Jf ni sehemu ya kujifunza mambo mengi muhimu sio kufuatiliana I'd ......
 
Back
Top Bottom