Wanaume kwa wanawake kwa mahitaji ya sexy lingerie kwa plus size nataka kujaribu hili soko

Wanaume kwa wanawake kwa mahitaji ya sexy lingerie kwa plus size nataka kujaribu hili soko

wa zion

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2013
Posts
223
Reaction score
481
Wasalaam wakuu,

Wanawake wengi waliojaliwa neema za Mungu mara nyingi wanapata shida sana katika kupata nguo nzuri za ndani(chupi na blazia) ambazo na yeye zitamfanya ajisikie vizuri kama wenzetu wenye miili size ya kati ambao nguo zao ni rahisi kupata na kwa bei nafuu.

Mara nyingi kama tukipata inaweza kuwa haina quality nzuri au bei huwa ni kubwa sana kiasi kwamba utashindwa kuhimili gharama au itabidi uwe na moja au chache kuendana na kipato chako.

Tatizo hili limekua kubwa kiasi kwamba hata kwa wenye ndoa kunakua hakuna muhamasiho wa tendo la ndoa kwa mume kutokana na nguo za ndani ambazo nyingi zinakua hazivutii maana kila siku mume anakuona na michupi yako ile ile haubadiliki imefikia muda mume amekariri atakukuta na blazia gani na chupi gani (mawazo yangu) .

Hivyo nikiwa mmoja wa muhanga wa tatizo hili la kukosa nguo za ndani ambazo zitanifanya nijisikie vizuri juu ya jinsi Mungu alivyoniumba nimeona ni bora kulitatua tatizo hili kwa kuleta suluhisho kwa sisi vibonge (we can be sexy too) waswahili huwa wanasema lifanye tatizo lako kuwa chachu ya mafanikio yako.

Wanaume kwa wanawake kwa mahitaji ya sexy lingerie kwa plus size nataka kujaribu hili soko najua vibonge humu tupo na wale wenye wake vibonge mpo na vibonge hatuna roho mbaya tutasapotiana tu.

NB: Kwa anaejua soko zuri ambapo nitapata nguo za ndani za wanawake wanene kwa bei nafuu tafadhali karibu DM
 

Attachments

  • plus size 2.jpg
    plus size 2.jpg
    15.8 KB · Views: 76
  • plus size 3.jpg
    plus size 3.jpg
    9.6 KB · Views: 82
  • plus size 4.jpg
    plus size 4.jpg
    45.3 KB · Views: 72
  • image.jpg
    image.jpg
    8.9 KB · Views: 101
  • plus size lingerie.jpg
    plus size lingerie.jpg
    7.4 KB · Views: 80
  • plus size.jpg
    plus size.jpg
    6.8 KB · Views: 72
Ukilipata soko tushituane na pia huku mbeya mabonge itakuwa ndo soko haswaa.Kama utakuwa unauza wewe safi zaidi.
Safi sana,wengine tuna aleji na vipotabo[emoji23]
 
Back
Top Bottom