Wanaume maskini, wenye elimu na upeo mdogo wa kufikiri kutoka jamii duni ndiyo hukataza wake zao kufanya kazi za Uzalishaji


Zama hizo zimepita Mkuu.

Yaani kama utakubali binti yako akiolewa asifanye Kazi aiseeh huyo binti atakuwa na bahati mbaya Sana kuwa na Baba wa aina yako.

Yaani binti ategemee ndoa kuendesha maisha yake?
Inasikitisha sana
 
Yaani Karne ya 21 ni ajabu kukuta bado kuna watu wenye mtazamo wa mwanamke asifanye Kazi za uzalishaji.
Ajabu sana
Wewe ndo waajabu watu wanahama kutoka huko wewe ndo unaona kimbilio, kufanya kazi kwamwanamke kuna impact ndogo kuliko faida yake......chanzo cha broken families ndo moja matatizo hayo
 
Zama hizo zimepita Mkuu.

Yaani kama utakubali binti yako akiolewa asifanye Kazi aiseeh huyo binti atakuwa na bahati mbaya Sana kuwa na Baba wa aina yako.

Yaani binti ategemee ndoa kuendesha maisha yake?
Inasikitisha sana
Mkuu maamuzi yake kwenye atakae muoa sio mimi kumuamlia. Ila jambo muhimu kwa mwanamke ni kutunza familia nyumbani sio kuzunguka barabarani kuuza bidhaa.
 
Wewe ndo waajabu watu wanahama kutoka huko wewe ndo unaona kimbilio, kufanya kazi kwamwanamke kuna impact ndogo kuliko faida yake......chanzo cha broken families ndo moja matatizo hayo

Familia zinavunjika kwa sababu ya akili za kibinafsi.

Wanaume tunapenda umungu mtu. Ndio maana wengi wanataka wanawake wasio na Kazi ili wawaburuze hata kwa mambo ya kijingajinga.

IPO wazi kuwa mwanamke akiwa na Kazi hawezi kukubali ujingaujinga au kuburuzwa kwa mambo ya kijinga na mwanaume.
Mfano, mwanaume umekosea au wewe unajipa uhalali wa kufanya uovu kwa gharama za uvumilivu WA Mkeo. Hiyo sio HAKI.

Ndio maana mwanamke akishakuwa na Kazi huwezi mletea upuuzi akakuchekea. Kama vile wewe ambavyo hutokubali Mkeo akuletee upuuzi ukamchekea.

Ni aidha ubadilike au ndoa ivunjwe na ndivyo inavyotakiwa.
 
Ndugu muandishi haya uliyoyaandika hapa yalipaswa kubakia kama mtazamo wako tu pekee na wengine mnaofanana kwenye mtazamo huo lakini sio kuwahukumu na kuwasema vibaya watu wengine ambao wapo kinyume na mtazamo wako kwani watu tumetofautiana kifikra.......

Lugha uliyotumia kama kichwa cha habari kimeshusha hata hadhi ya msingi wa hoja yako pengine ingekuwa na mashiko na kuchukua fikra za watu kama ingebakia kuwa mtazamo wako na watu watoe maoni Yao....

Hata hao wanaokemea wenza wao kufanya kazi na wao wana hoja zao za msingi na haziwezi kukubalika na wote kwani huo ndio ubinadamu wenyewe.......

Lugha uliyotumia unaonesha jinsi gani ubishani wako wa hoja ulivyo duni na unaishi kwenye boksi la fikra zako Tu........

MSAWAZO KWENYE JAMII INALETWA KUSHIMIANA NA KUKUBALI KUTOFAUTIANA PASI NA KUVUNJIANA HESHIMA...
 
Mkui maamuzi yako kwenye atakae muoa sio mimi kumuamlia. Ila jambo muhimu kwa mwanamke ni kutunza familia nyumbani sio kuzunguka barabarani kuuza bidhaa.

Sio lazima azunguke kuuza bidhaa Kazi zipo nyingi.

Ndio maana tukasema kwa watu wabinafsi iko Sawa kwao.

Lakini kwa wababa wenye upendo na wanaojali hawatakubali kuona binti yao anaenda kuwa mtumwa wa mtu mwingine ambaye wanaweza kuachana muda wowote kwa kile kiitwacho ndoa.
Yaani binti yangu asifanye Kazi ili umtese Hilo labda niwe nimekufa kwa kweli
 
Kwani lengo la kuoa ni kupata mshindani wa maisha rafiki yangu Robert mbona anataka ku-reason kama "feminist" wakati na kuaminia kwa mada zingine ila sio hi, hamna mwanaume anaependa ligi nyumbani kwake always husband is above a wife
 

Kazi ni HAKI ya msingi kwa mtu.
Hakuna lugha nyingine ningeweza kutumia zaidi ya lugha Kali kwa watu wanaonyima HAKI hiyo.

Ni Sawa uniambie ntumie lugha rafiki kukemea ukeketeja, au ndoa za utotoni kisa kuna watu wenye mtazamo tofauti na wangu.

Kumzuia mtu kufanya Kazi ni uhalifu, uovu, n kumnyima Uhuru mtu huyo na kumfanya tegemezi na mtumwa. Bado unataka niongee kwa Lugha ya kuperemba?
 
Kwanini waachane hizo juhudi za kufanya kazi zielekeze kwenye upatanishaji wa ndoa wakae sehemu moja, usiwe hasi mkuu.
 
Kwani lengo la kuua ni kupata mahindani wa maisha rafiki yangu Robert mbona anataka ku-reason kama "feminist" wakati na kuaminia kwa mada zingine ila sio hi, hamna mwanaume anaependa ligi nyumbani kwake always husband is above a wife

Mwanaume ni kichwa cha familia lakini hiyo haiondoi HAKI ya mwanamke kufanya Kazi?

Alafu ninyi ndio baadaye mnasema kwenye kugawa Mali wasipewe 50*50 za Mali. Alafu mliwazuia kutafuta Mali.
Hivi kuna ubinafsi na ukatili zaidi ya huo?
 
Mwanaume ni kichwa cha familia lakini hiyo haiondoi HAKI ya mwanamke kufanya Kazi?

Alafu ninyi ndio baadaye mnasema kwenye kugawa Mali wasipewe 50*50 za Mali. Alafu mliwazuia kutafuta Mali.
Hivi kuna ubinafsi na ukatili zaidi ya huo?
Hiyo "Haki" ya kufanya kazi unaitoa kwenye kitabu gani?
 
Kwanini waachane hizo juhudi za kufanya kazi zielekeze kwenye upatanishaji wa ndoa wakae sehemu moja, usiwe hasi mkuu.

Kuachana ni lazima Mkuu.
Kuachana kupo.
Kuachana kwa Kifo au Talaka.

Ni mjinga tuu asiyefikiria au asiyejua kuwa IPO siku ataachana na mkewe/mumewe.
Kama mlikutana siku moja basi IPO siku mtaachana iwe kwa kupenda au kutokupenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…