Wanaume maskini, wenye elimu na upeo mdogo wa kufikiri kutoka jamii duni ndiyo hukataza wake zao kufanya kazi za Uzalishaji

Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume
Ndo maana nakwambia majukumu ya mama ni mzazi na mlezi
Mwanamke anakaa nyumbani anajali mifugo kwani mifugo sio pesa
Analeta watoto

Kumfanyisha kazi mwanamke ndo kumdhalilisha zaidi kuliko kumpa heshima

Kwani wapi nimekataa mwanamke sio mama mzazi na mlezi?

Kwa mwanaume si ni mzazi na mlezi pia?

Embu tuambie mwanamke aliyeachwa na mumewe Nani anaowajibu wa kumtunza yeye na watoto wake?

Embu eleza mwanamke ambaye hajaolewa Nani anaowajibu wa kumlea?

Embu eleza mwanamke mjane ambaye hajazeeka Nani anaowajibu wa kumtunza na kumhudumia?

Embu eleza, mwanamke ambaye mumewe hataki kutoa mahitaji ya nyumbani, au huduma za nyumbani ni DUNI. Nani wakusaidia kiuchumi hapo nyumbani kama sio mke?
 
Sitaki afanye kazi nataka aishi kama Queen pesa zote nilizotafuta kwanini na yeye ateseke?
 
Sitaki afanye kazi nataka aishi kama Queen pesa zote nilizotafuta kwanini na yeye ateseke?

Kufanya Kazi sio kuteseka.
Kazi ni IBADA.

Ni Sawa useme, ninavyoswali hivi na kufunga Ramadhan hivi kwa nini mkeo au watoto wako nao wafanye hivyo.

Kazi ni HAKI ya mtu kama HAKI zingine.
 
Huyu kwenye suala la ndoa anaonekana hajui kitu, afahamu tu kuwa maisha ya ndoa hayana shule! Kila wanandoa wana mtindo wao wa maisha. Hakuna fomula moja ya ndoa! Pengine hiyo ndio fomula yake sasa asilazimishe wanandoa wote wakaishi kama yeye!
Ni dogo janja ambaye hajawahi ishi na mwanamke siunaona anaandika ujinga ujinga
 
Hawa viumbe uhuru ukizid tegemea maajabu makubwa sana kwenye ndoa , hawa ni wakuwekewa mipaka na wakuchungwa nama mbuzi tu,
 
Uanaume ni silika na tabia. Naona vijana wengi wa kiume lakini hawana tabia za kiume.

Umbile la mwanamke kiasi ni kukaa nyumbani. Ona vurugu na madhila ambayo yapo Sasa kutokana na mwanamke kutafuta pesa.
 
Umemaliza kila kitu kwenye huo mjadala, Kuhudumia familia ni jukumu la mwanaume sio la mwanamke, mwanamke hata akiwa anafanya kazi au kua na kipato kikubwa suala la Kuhudumia familia linakuwa hiyari yake. Halafu hiki kizazi cha sasa hivi sijui kina tatizo gani kinapenda sana mserereko, yani unakuta mwanaume mzima amekaa anapigia hesabu hela ya mwanamke.
 
Yaani Karne ya 21 ni ajabu kukuta bado kuna watu wenye mtazamo wa mwanamke asifanye Kazi za uzalishaji.
Ajabu sana
Asili haiathiriwi na wakati kijana. Hivi huwa mnatumia nini kuyaangalia haya mambo ? Au mnaandika tu mjifurahishe.

Hakuna mwanaume mwenye tabia za kiume akaandika haya unayo yaandika.

Inaonekana humjui mwanamke vizuri.
 
Wewe jamaa saikolojia yako inakutuma vibaya. Kwahiyo wewe unajua sana kushinda Mungu aliyesema utazaa kwa uchungu. Maaana yake ni kuzaa na kulea. Na wewe mwanaume utakula kwa jasho. Ni kuipatia mahitaji familia.

Kwa mtizamo wako huu mbovu WAARABU wote ni maskini. Hii kazi inakushinda
 
Asili haiathiriwi na wakati kijana. Hivi huwa mnatumia nini kuyaangalia haya mambo ? Au mnaandika tu mjifurahishe.

Hakuna mwanaume mwenye tabia za kiume akaandika haya unayo yaandika.

Inaonekana humjui mwanamke vizuri.

Asili ipi unaizungumzia?

Kumjua au kutomjua mwanamke kuna uhusiano gani na HAKI yake ya kufanya Kazi kama MTU?
 
Uanaume ni silika na tabia. Naona vijana wengi wa kiume lakini hawana tabia za kiume.

Umbile la mwanamke kiasi ni kukaa nyumbani. Ona vurugu na madhila ambayo yapo Sasa kutokana na mwanamke kutafuta pesa.

Kwa uelewa wako Kazi zote zinamadhila au zinatumia nguvu?
Kwa uelewa wako lakini.
Kumaanisha tangu kuzaliwa na mazingira yako wewe umekutana na kuzijua tuu Kazi zenye madhila, vurugu na zinazohitaji misuli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…