Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amekopi na kupest storyKuna watu mna mioyo...unakaa na huo mzigo wa maumivu na majuto mpaka lini?
From FBcopy and paste
From FBAmekopi na kupest story
Japo huwa kuna mambo kama hayo....kuna mambo yanatokea unashuhudia unashangaa hivi kumbe ni kwelii!From FB
Yeah ni kweli inatokea hio kwa baadhi ya watu,Japo huwa kuna mambo kama hayo....kuna mambo yanatokea unashuhudia unashangaa hivi kumbe ni kwelii!
Mdogo wangu mmoja tulisoma vidato yeye akiwa nyuma alifika udom akaruka ruka tayariii alivojifungua tu mama ake akachukua mtoto wakaenda kumficha na akaonywa eti nsije kuskia unasema una mtoto, na yule kijana alozaa naye akaonywa asije sema kama kazaa na binti yao, wachumba walikuwa wakija kuchumbia bahati nzuri bana hakuna siri ya wawili wakigundua kuna iyo siri wanamuachaYeah ni kweli inatokea hio kwa baadhi ya watu,
Sio zake huyu jamaa ndo mana zinafukiwa tu kulinda ndoaUnajuaje Kama ni zako?
Numbe copy and paste. LohNIFANYE NINI MKE WANGU AMETOA MIMBA ZANGU TANO?
Mimi ni kijana wa miaka 33, nimeoa na ndoa yangu ina miaka mitatu sasa. Ndoa yangu ilikua nzuri sana na tangu kuingia kwenye ndoa mimi na mke wangu tulikua tuko vizuri tu. Lakini lilikuja suala la kupata mtoto, kila tulipokua tukihangaika kupata mtoto ilikua ni shida sana, tulishapimwa mahospitalini na kuonekana wote hatuna tatizo.
Kwakua naamini katika Mungu nilikubaliana na ukweli kuwa ni mipango yake hivyo nikaamua kukaa kimya na kusubiri majibu. Wiki iliyopita mke wangu alianza kuumwa, alikua anaumwa sana tumbo, nilitaka kumpeleka hositalini akawa hataki, akaniambia kuna dawa amekunywa atajisikia vizuri.
Lakini hali yake haikua nzuri kabisa, alikua anazidi kuumwa tu, nililazimishia kwenda hospitalini ila aliniambia kuwa yuko sawa na kweli usiku huo alipata usingizi. Wakati akiwa kalala kuna meseji iliingia kwenye simu yake, mimi na mke wangu tunaaminiana, anashika simu yangu na mimi nashika yake.
Ilikua ni meseji ya rafiki yake na alikua anamuuliza kama anaendeleaje, huwa sina kawaida ya kusoma meseji zake kwani namuamini sana, lakini ile niliiona kwa juu na kwakua nilikua najua ni watu wanapendana ni marafiki basi niliona hakuna shida kumjibu kuwa angalau kapata usingizi. Niliifungua ile meseji na katika kujibu niliona meseji za juu yake.
“Yule Daktari hayupo, amefiwa na mke wake kasafiri, usiende Hospitali kwani ukienda kwa daktari mwingine mume wako atajua kuwa umetoa mimba, vumilia shogaa, kunywa hata vidonge vya usingizi asubuhi nitakupeleka mimi.” Meseji ya nyuma ilisema hivyo, mke wangu alijibu “Sawa lakini najihisi hata kufa, natamani kumuambia mume wangu kuwa sitaki mtoto tena.” Mke wangu alimjibu “Ukimuambia hivyo anakuacha mwenzako hana mtoto angalau wewe una wawili…”
Rafiki yake alimjibu hivyo na mke wangu hakujibu tena, meseji za nyuma kabisa zilikua zimefutwa. Kusema kweli nilihisi kuchanganyikiwa, sikutaka kuamini kuwa mke wangu ambaye tumekua tukihangaika mwaka watatu kutafuta mtotoametoa mimba, ilikua haiingii akilini pia kujua kuwa mke wangu ana watoto wawili, niliumia sana lakini sikusema chochote.
Niliscreenshot zile meseji na kujitumia, kisha nikafuta meseji ya rafiki yake ambayo alikua anaulizia hali yake ilia sijue kama nimeziona na sikumjibu tena rafiki yake. Asubuhi nilimuamsha mimi, na kumuambia kuwa nataka twnede hospitalini, aligoma lakini sikukubali, nilimuambia kabisa kuwa siwezi kumuacha afe kisa tu anaogopa kwenda hospitalini. Nilimsimamia akajiandaa nakumpeleka hospitali mimi mwenyewe.
Hakutaka niingie neya kwa Daktari kama kawaida yetu lakini sikujali, nilimpeleka kwa Daktari ambaye nafahamiana naye na nilishamuambia usiku kuwa nahisi kuna kitu kama hicho. Aliingia na kufanyiwa vipimo, kweli alikua katoa mimba na alikua hajasafishwa vizuri. Nilimhudumia mpaka nikahakikisha amepona, sikuongea kitu chochote na wala sikumuuliza kama alikua anaumwa nini, aliniambia tu tumbo lilichafukwa basi nikakubaliana naye.
Nilikaa kimya na kuanza kuchunguza vizuri, haikua shida kwani ndugu zake walikua wanajua kuwa najua ana watoto. Nilimtafuta tu mdogo wake, nikamtopa out na kuanza kuulizia habari za watoto wa dada yake kwani nilikua nahitaji tuwachukue.
“Unajua Dada yako anakua mpweke sana, hajanaimbia kuhusu kuwahcukua watoto ila nahisia naogopa, nataka nimfanyie sapraizi….” Nilimuambia.
Hapo ndipo alifunguka kuwa Dada yake alikua na watoto wawili ambao alizaa na wanaume tofauti na watoto wote wapo kwa Baba zao, hivyo hadhani kama hao wanaume wanaweza kumpa watoto. Aliniambia kuwa Dada yao ndiyo aliwapeleka alipokua chuoo akawatelekeza huko , ila baada ya kupata kazi alitaka kuwachukua Baba zao wakagoma ndiyo maana hakuhangaika nao tena, aliniambia labda niongee na Mama yake anaweza kunisaidia.
Mimi nilimuambia basi asimuambie Mama yake nitajua kitu cha kufanya lakini kusema kweli mpaka sasa hivi nimechanganyikiwa. Bado sijamuambia mke wangu kama najua kwua ana watoto, kibaya zaidi nimechunguza naklugundua kuwa ile mimba haikua ya kwanza, mke wangu alishatoa mimba zangu tano kwakua tu hataki mtoto kwa wkaati huo, nashindwa kuelewa nifanye nini, nachanganyikiwa sijui nimuulize mke wangu au nifanye nini, naomba ushauri wako ndugu.
copy and paste