Wanaume Mkoa wa Njombe Wanatozwa Fedha na wake zao kupata tendo la ndoa

Wanaume Mkoa wa Njombe Wanatozwa Fedha na wake zao kupata tendo la ndoa

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Diwani wa Kata ya Ramadhani, Erasto Ngole amesema kumekuwepo na changamotoya kijamii katika eneo hilo ambapo baadhi ya wanawake wanadaiwa kuwatoza fedha waume zao kabla ya kuwapatia tendo la ndoa.

Ngole amesema hadi sasa ofisi yake imepokea jumla ya kesi tano zinazohusiana na suala hilo, hali ambayo amesema inaashiria kuibuka kwa mwenendo unaohitaji uchunguzi pamoja na utoaji wa elimu kwa jamii.

Diwani huyo amesema wanawake wanadai kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kugundua kuwa waume zao wamekuwa wakitumia fedha nyingi kuwagawia wanawake wengine nje ya ndoa.

"Lakini sasa ukiwauliza vizuri akina mama, akina mama wanasema: "Tumeamua tu tuwe tunawatoza kwa sababu tunajua wakienda nje kule baa wanatoa hela. Kule nje, kule nje wanatoa Sh20,000, Sh15,000, Sh10,000 na akina mama sasa wanataka na wenyewe kulipwa."

Ameeleza kuwa baadhi ya wanaume wanashindwa kutekeleza majukumu yao ya kifamilia, ikiwemo kutoa mahitaji muhimu ya nyumbani yanayofahamika kama “kodi ya meza”, jambo linalodaiwa kuchangia migogoro ndani ya familia na kusababisha makubaliano yasiyo ya kawaida kati ya wanandoa.

Aidha, ametoa wito kwa jamii kuendelea kujenga maelewano ndani ya familia na kutatua changamoto za ndoa kwa njia ya mazungumzo ili kudumisha amani na mshikamano wa kifamilia.

"Kwahiyo jamani, ili mambo yaende ni lazima tutunze na tuache hela ya chakula na mahitaji nyumbani kwa wake zetu. Na wakati mwingine hata akina mama kuchepuka, sisi ndio tunaosababisha. Sasa kama anajua kabisa wewe hutoi hela, na akienda mlango wa pili atapata hela, lazima naye ataenda kuchepuka."

"
 
Hehe! Kila siku tunajadili wa iran kumbe tunao wa iran hukuhuku wanazuia mfereji wa Hormuz mpaka wapewe sasampa!!, haka ka nchi kangu ndani yake kuna ka nchi kadogo!, kunamambo yanaweza yakawa yanaendelea halafu usijue mpaka yaibuke...😅
 
wanaume wengi tuTanzania wanatozwa fedha na wake zao kupata tendo la ndoa. Ni kwamba tu wanapuuza ile cost incurred ila kutozwa kupo kila sehemu.
 
Bora kutozwa hiyo 5,000 kuliko kugomewa bila sababu za msingi. Dunia inaenda kasi sana.Ukiwa na 5,000 uwakika, ukiwa huna huangaiki kuomba. hyo.Namahari ulitoa.Nimeipenda hiyo.
 
Njombe Njombe Njombe
Nimewaita Mara Tatu
 
Back
Top Bottom