Tajiri wa kusini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,079
- 2,947
WANAUME MNA NINI LAKINI ?
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂
Nina umri wa miaka 24 Nina mtoto mmoja baba wa huyu mtoto wangu nilikuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka kama mitatu hivi.
Ni mwanaume ambaye nilimpenda kweli mpka nikawa namsaidia akiwa na changamoto kipindi hicho nilikuwa chuo wakati tunaanza mahusiano japo yeye hakuwa mwanachuo na alikuwa mkoa mwingine tofauti na nilipokuwa nasomea, na mimi nilikuwa na malengo yangu ya kukusanya mtaji nikawa nabana mkopo wangu sasa alipojua tu nimeweka akiba akaanza kama kunikopa ili anirudishie ila hajawahi kurudisha ikifika muda tuliokubaliana kurudisha analalamika changamoto nikawa namwonea huruma nikaacha kumdai akawa ananiambia mimi ndo mke wake kwahiyo hata tukifanya vitu kwa pamoja haina shida maana ni kwa ajili yetu badae na watoto wetu.
Alikuwa mwanaume wangu wa kwanza ila hajatulia kabisa mara nyingi nakuta SMS zinazoonyesha ana mahusiano mengine na siyo mwanamke mmoja ni wengi tu, nikimuuliza anakana hata kama ushahidi upo hapo hakubali kama ana mahusiano mengine na kila nikisema niachane naye nilikuwa nashindwa mpaka nilipopata ujauzito wa huyu mtoto matukio yalizidi kwanza alipunguza mawasiliano akawa anadai yuko bize hana muda na mimi.
Nilipojifungua akaanza kujirudi sasa kumbe kuna mwanamke mwingine tena ana mimba yake nilipomuuliza akaniambia mwanamke alimtegeshea lakini yeye hana malengo naye.
Mie nilimwambia tuachane nimechoka kuumia kila mara hataki kusikia hicho saivi kaanza kunyenyekea anasema hawezi kuishi bila mimi ila simuamini hata kidogo maan ni muongo sana ni mtu mwenye ahadi nyingi ila hajawahi kutimiza hata moja.
Mtoto anahudumia pale anapoweza ila ni kama vile hajali nikimwambia mtoto anaumwa atasema tu pole na hana tabia ya kusema ngoja niulizie huyu mtoto anaendeleaje hauliziagi alafu anadai bado ananipenda na anataka kunioa.
Hivi hapo kuna upendo kweli ??