Wanaume mnakwama Wapi? Vunja Vikoba Dar Desemba 2020

Wanaume mnakwama Wapi? Vunja Vikoba Dar Desemba 2020

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Habari za jioni,

Natumai hamjambo, mko poa na mnaendeleza gurudumu la maendeleo.

Tangu mwezi wa 11 mwaka huu 2020 kumekuwa na wimbi la wadada/ wamama kuvunja vikoba vyao kwa maana ya vikundi vya wakina dada/mama hawa kukutana wanaenda mahala na kufurahi pamoja.

Kawaida vikundi hivi vya kina mama au dada huwa na malengo maalum, mojawapo kusaidiana kwenye shughuli zetu za kiafrika. Harusi, misiba, graduation, kupata mtoto, na kadha wa kadha.

Ili kukabiliana na gharama za kupongezana huko kunakuwa na michango ya kila mwezi, baadhi ya vikoba hukopeshana na riba inayopatikana ndo wanachama hugawana mwisho wa mwaka. Vikundi hivi huweka mikakati ya kukutana aidha kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu. Mwanachama asiyehudhuria kikao anapigwa fine inajazia mfuko wa chama.

Kqenye vikundi hivi vya kina dada kuna mengi, kuna ambao wamekutana wako vizuri wao ni kula bata tuu na kusafiri mahala mahala for fun.

Kuna ambao wao hupeana malengo ya kutimiza mfano kujiendeleza kielimu, kupeana michongo ya hela, kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora kwa kuwapeleka shule nzuri, kununua viwanja na kujenga, wengine kuwekeza kwenye soko la hisa na kupeana moyo kuhakikisha kila mwanachama anatimiza malengo yake.

Wako wanaogombana, wako wanaojenga ukaribu hadi kuwa sehemu ya familia zao n.k.

Wengi wa wadada hao mwisho wa mwaka wanapovunja vikoba huandaa sare za nguo, hudamshi, wanaandaa usafiri wa kuwapeleka wanakoenda na kufurahia / kupongezana umoja wao.

Wengine hufanya mkusanyiko wa siku moja na jioni yake kika mmoja kurudi makwao na wengine husafiri nje ya mkoa wanaoishi.

Kuna kikoba kilishaenda Egypt, wengine serengeti national park tour, wengine Nairobi, wengine zanzibar basi kila kikoba na matakwa na uwezo wao.

Wadada hawa ni mchanganyiko wa walio single na walio olewa. Ila wakitoka huwa wanajua kupendeza aisee.

Najiuliza tuu, wanaume / wakaka mnakwama wapi?

Kuna status za whatsapp zimekuwa zikipita kjwa wanaume tulia nyumbani huu ndo muda wa kumsikiliza mkeo maana vikoba vinavunjwa mwisho wa mwaka huu.
Najua ni utani si kuwa wanaume wanategemea hela za vikoba za wapenzi/ wake zao (japo kuna ambao wapo).....

Wanaume, hampati ushawishi / hamu nanyi kuwa na vikundi vyenu mkawekeana malengo ya kujiendeleza kielimu, kujenga, kusafiri, connection ya kazi na biashara n.k.

Natamani kuona wakaka wametoka on their own having fun wakipongezana kwa malengo waliyowekeana mwanzo wa mwaka baada ya kuyatimiza na yale ambayo hayajatimizwa kuweka mikakati mipya namna ya kuitimiza.

Najua baadhi ya wanawake wanaendesha familia zao kwa hivi vikoba na wengine wanasema wanamabwana, yawezekana lisemwalo lipo ila wengi nnaowafahamu vikoba vinawaweka mjini ukijumlisha na kampani.

Wanaume/ wakaka vikoba viipiii?

Kati ya hizo picha mmojawapo ni Kasinde.

Kasinde Matata 2020.
 
Tunavunja alhamis K’Matata.

Vipi na wewe chenu mmeshavunja

Hivi hawanaga kweli!!!???

Wanaume njooni huku

Ooh kila la kheri dear.

Sie tulishavunja tulienda Zanzibar siku kadhaa. Ilikiwa raha hadi raha yenyewe ikachukia aahahahahahaaa.

Sijawahi sikia wanaume wakiwa na vikoba na kama wanacho basi wanafanya kimyakimya.

Labda wanavivunjia Bar 😅

Wakuje watushirikishe nasi tujifunze kutoka kwao, hasa kwa vile vikoba vinavyokuwaga na ugomvi mara kwa mara.
 
Ooh kila la kheri dear.

Sie tulishavunja tulienda Zanzibar siku kadhaa. Ilikiwa raha hadi raha yenyewe ikachukia aahahahahahaaa.

Sijawahi sikia wanaume wakiwa na vikoba na kama wanacho basi wanafanya kimyakimya.

Labda wanavivunjia Bar 😅

Wakuje watushirikishe nasi tujifunze kutoka kwao, hasa kwa vile vikoba vinavyokuwaga na ugomvi mara kwa mara.
😘😘😘🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️

Wow hongereni sana.

Ehee wanakuwaga na vile vikoba vya totoz wanavivunjaga kila mwisho wa mwezi baa 😆😆😆😆
 
😘😘😘🧚‍♀️🧚‍♀️🧚‍♀️

Wow hongereni sana.

Ehee wanakuwaga na vile vikoba vya totoz wanavivunjaga kila mwisho wa mwezi baa 😆😆😆😆

Yaaani hivo kila wiki ijumaa wanavunja vikoba na totoz looh 😜
 
Vacation yetu ni BAR na inatosha.

Sie kila weekend tunavunja hivyo vikoba na tena hasahasa mwisho wa mwezi na kukutana bar na kupeana connection za kiume.

Mwendo wa kugonga toast [emoji485][emoji485][emoji485] tukitoka hapo ni kufunguliwa mlango nyumbani ,tunawapa hi watoto, mnatupakulia chakula then tunawala na nyinyi.

Nb. Huko ulaya tunaenda kwa ziara za kikazi. Period!!!
 
Vacation yetu ni BAR na inatosha.

Sie kila weekend tunavunja hivyo vikoba na tena hasahasa mwisho wa mwezi na kukutana bar na kupeana connection za kiume.

Mwendo wa kugonga toast [emoji485][emoji485][emoji485] tukitoka hapo ni kufunguliwa mlango nyumbani ,tunawapa hi watoto, mnatupakulia chakula then tunawala na nyinyi.

Nb. Huko ulaya tunaenda kwa ziara za kikazi. Period!!!

Wewe umesema ukweli...

Acha sie wadada tuendelee kujipa raha na vikoba vyetu, mwakani tumepanga kwenda Zambezi Falls korona akienda zake.
 
Vikoba vimeshahusanishwa na akina mama kiasi cha kwamba mwanaume ukiwemo waja wanakuangalia mara mbili mbili
 
Back
Top Bottom