Wanaume mnaweza kulia kwa habari tofauti na ya msiba?

Wanaume mnaweza kulia kwa habari tofauti na ya msiba?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Ukiwa mwanafunzi kweli unaweza ukapigana shuleni ukahisi umeonewa ukatoa machozi. Lakini kwa mtu mzima aisee nimeshindwa kutoa chozi labda nilie msibani ila hata Kama nyumba yangu au duka lije kuungua moto never siwezi kulia kamwe.

Hata Kama nifungwe bila hatia siwezi kulia. Labda nyie mniambie ni Jambo gani linaweza kumfanya mtu mzima akaumia mpaka akatoa machozi au ni mapenzi yamekufanyaje mpaka ulie kusalitiwa tu au ni nyimbo za kuabudu zikuguse ndo ulie?

1633329395355.jpeg
 
Hapo ulipo jiulize ni mtu gani unampenda sana amekuingia sana moyoni. Anaweza akawa mamaako,babaako,mtoto wako. Yoyote namba moja moyoni mwako akakata moto ghafla iwe kwa ajali au vyovyote. Utalia sana,tena hutaamini
 
Shukuru Mungu kuwa hulii mkuu. Si kila anaemwaga machozi hupenda. Halijakukuta bado na Mungu akuepushie yasikukute.
Si kila unachohisi ndio cha muhimu sana kukipoteza ndio pekee kinaweza kukutoa machozi. Mara nyingi vilizavyo ni vile uvianavyo vidogo sana na kuvidharau.
 
Back
Top Bottom