Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Leo hii ndoa nyingi sana zimeingiliwa na kujihami kwa aina mbalimbali, lakini aina kubwa au inayofanywa sana ni ile ya kuhamisha (Displacement). Kwa mfano, mabosi wetu wanapotuudhi ofisini, tunaweza kuhamisha hasira zetu kwa makondakta wa daladala. Tunafanya hivyo ili kupunguza maumivu, kwani tusingeweza kukabiliana na mabosi wetu, hivyo tunatafuta shabaha dhaifu zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanatumia njia ya kujihami ya kuhamisha kwa kiwango kikubwa sana. Wanaposhindwa kupanda vyeo, wanapotishiwa kufukuzwa kazi au kampuni kufungwa, wanapopata hasara kwenye shughuli zao, ‘tenda' zinapokataa na mengine kama hayo, hutafuta mahali pa kupeleka hasira zao. Kwa sehemu kubwa hasira hizi hupelekwa majumbani kwa wake na watoto wao. Kwa hiyo baba au mume anatokea kuwa mkali, mwenye maneno na kauli chafu nap engine hata kupiga. Ukichunguza utagundua anajihami kupunguza maumivu ya kile kinachotokea kwenye shughuli zake. Wakati mwingine hata timu aipendayo inapofungwa, mume au baba huwa mkali sana na hata kupiga watoto au kuropoka kwa mke.
Hii ni hatari sana kwa familia zetu, kwani watoto huingia kwenye kuchanganyikiwa na wake nao huhisi kwamba, hakuna tena upendo. Mbaya zaidi ni kwamba, watoto watakuja nao kuishi hivyo kwenye ndoa zao. Ndoa nyingi hivi sasa zinakabiliwa na hali hii ya waume kujihami kwa mtindo huu wa kuhamisha. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko au kasi ya mabadiliko kijamii, kiuchumi na hata kisiasa. Mambo yanazidi kuwa magumu na dunia inazidi kuwa ndogo na kuwaminya wengi. Hapo ndipo binadamu wanazidi kupoteza subira zao. Moja ya sababu ya kubwa ya wanaume kuwasimanga wake zao, kuwatolea kashfa mbaya, kuwajibu kwa mkato, hata kuwapiga, ni hii ya kujihami. Ndiyo njia pakee kwa sasa kwa wanaume wengi kuwapa taarifa wake zao kwamba, mambo ni magumu. Wanaume hawa huhalalisha wanachofanya, kwa sababu hawajui kwamba, kinachotokea ni kutafuta namna tu ya kujihami, wasiumie zaidi kwa kile kinachowasibu huko nje. Lakini wanaumiza ndoa na familia zao.
Inashauriwa mambo ya nje ya nyumbani yaishie kizingitini. Mtu akiingia nyumbani kwake ajaribu kuwa mwanga wa nyumbani na siyo giza na kitisho kwa wale anaowaita wapendwa wake. Lakini wanawake nao pia wanaaswa kujua kwamba, wanaume hivi sasa wanaishi kwa kujihami, badala ya kuwa wakweli. Kauli chafu, maneno ya kejeli na masimango, wakati mwingine ni majibu au maelezo ya waume kwa wake zao kuhusu hali wanayoipata huko nje.