LadyAJ
JF-Expert Member
- Oct 21, 2015
- 7,173
- 9,642
Kwa ufupi tu
Tabia ya kuwa na mawazo mazuri, kuwaza mema na kulifikiria jambo kwa upande wa uzuri hutusaidia katika namna nyingi.
..........Swali la kujiuliza
1.Je, unaishi kwa kukubalika katika jamii?
2. Je, una maelewano na ushirikiano mzuri na jamii inayokuzunguka? Kama ndiyo unapata faida au manufaa gani kutokana na maelewano na jamii inayokuzunguka?!
3.Kama hakuna maelewano na ushirikiano wa kutosha baina yako na jamii, unapata shida gani? Je, unafanya nini ili kutatua tatizo hilo.
FAHAMU KWAMBA Kamwe binadamu hawezi kuishi na kujitosheleza peke yake bila kutegemea watu wengine Katika maisha yetu ya kila siku kuna ukoo na jamii inayotuzunguka, Makundi haya ya kijamii ndiyo yanayotuwezesha kuishi maisha bora kwa maana Kama tutakuwa katika hali ya upweke, kukosa furaha na faraja tunaweza kuipata ikiwa tutakuwa na maelewano na uhusiano mzuri na jamii.Muda mwingine kama Binadam tunapitia magumu na hali ngumu lakini ikiwa unaishi vizuri na ndugu, jamaa na Marafiki zako unauwezekano mkubwa wa kupata ahueni ya faraja kutoka kwao
Yafuatayo ni baadhi ya Mambo yanayoweza kukufanya ukubalike na uishi vizuri na jamii
1. Tambua hadhi yako na changanyika na jamii
Moja katika mambo muhimu katika kujenga ushirikiano na jamii ni kuweza kuchanganyika na watu. Iwapo unaona vigumu kuchanganyika na watu, huenda ni kwa sababu hujajithamini wewe mwenyewe kiasi kinachostahili. Vile vile umeshindwa kubaini kiwango cha thamani yako katika kushirikiana na ukoo au jamii yako kutatua shida na changamoto mbali mbali na unajihisi hauna unachoweza kuchangia au unajipa hadhi ya juu sana inayokufanya ujione bora kuliko wao KUMBUKA BINADAMU WOTE NI SAWA NA MWISHO WA SIKU SOTE TUTARAMBA MCHANGA
2. Kuwa na hisia Na mawazo mazuri dhidi ya wengine
Kua na tabia ya mawazo mazuri, kuwaza mema na kulifikiria jambo kwa upande wa uzuri hutusaidia katika namna nyingi hasa tunapowafikiria vyema watu wengine tutaweza kupata suluhisho la mambo mbali mbali katika familia,ukoo na jamii kwa ujumla Watu wanapogundua unawathamini na wao watakupenda, hatimaye nyote kwa pamoja mnaweza kujenga uhusiano mtakaoufurahia
Mfano Unapoamua kwenda kwenye shughuli za kijamii kama harusi,misiba na hata sherehe nyinginezo au za ki kazi huna budi kujifunza kuiweka sura yako kulingana na shughuli husika kama ni sherehe basi jitahidi uso wako uonekane ni mwenye furaha kwa maana ukijipa ukisirani utaonekana kama vile umekwenda kubeza au kukosoa na watu watakuchukia sana
3. Epuka kujisikia kuwa wewe ni bora zaidi kuliko wengine
unapokuwa umejumuika katika kundi la watu. Kuna watu waliozoea kujifanya ni watu wa juu zaidi, hasa wanapokuwa mbele ya watu. Pengine hujikweza na kujionyesha wako juu kiasi kikubwa sana, wala hawastahili kuzungumza na watu wengine.Tabia hii huwafanya wengine wajihisi kuwa hawastahili kuzungumza na wewe . Hali hii ina madhara makubwa sana kwani watu wataamua kukutenga kwa madai kuwa una majivuno na unaringa jambo ambalo si zuri
4. Kuwathamini wengine
Jitahidi kila wakati kuwaonyesha watu wengine ishara zitakazowafanya wajihisi wao ni watu muhimu na wanahitajika. Ongea na watu kwa upendo na ukarimu na kila inapotokea fursa wakafanya jambo zuri uwasifu na kuwapongeza kwa dhati bila kuwakebehi.
"Kumbuka kadri unavyofanya watu wengine wajisikie vizuri ndivyo kadri na wewe utakavyojisikia vizuri hata zaidi kuliko wao na utabarikiwa Zaidi"
NB. Kuwathamini watu wengine na kukubali kuwa kuna kitu ambacho wao wanaweza kuwa wanakijua, ambacho wewe hukijui ni siri moja kubwa ya mafanikio katika kujenga uhusiano thabiti na jamii.
4. Kuwa na hulka iliyo rafiki
Jambo linalowapendeza watu katika jamii za aina zote ni mtu kuwa na moyo wa hisani na upendo kwa watu wote. Hisani huweza kukamilishwa kwa mtu kuonekana kwa tabia na mwenendo wake,Wewe ukiwa kama mtu unayetaka kukubalika katika jamii, jitahidi kila mara kuwa wa kwanza kusalimu watu, kupeana nao mikono na kuanzisha mazungumzo. Watu husema “Salaamu ndiyo mwanzo wa kujuana” Na Kuna msemo usemao "SALIMIA WATU PESA HUISHA" hivyo ni vyema tukajengeka katika kuona kila anayetuzunguka ni rafiki hata kama ni masikini kiasi gani!
Pia huna budi kuyafahamu na kutoyasahau majina ya watu. Kuyatumia kila unapoongea nao ni njia moja inayosaidia zaidi kujenga udugu na urafiki. Kwa kawaida hakuna sauti inayomfurahisha mtu kuliko sauti ya jina lake linapotajwa.
Napenda nimalizie kwa kusema kua, M/Mungu mkuu wa vyote Duniani alituumba binaadamu katika hali tofauti kama vidole vya mikono lakini alitupa mtihani mmojatuufanyao kila siku ili kutukumbusha kua pamoja na utofauti wetu sisi bado ni wamoja na ndio maana TAJIRI NA MSIKINI WOTE KUNYA.