1.Uzuri ni subjective....fafanua - kuna uzuri wa sura ambao ni subjective, kuna uzuri uliojificha ambao hujakuonekana baada ya muda.Sasa utafanyeje kwenye hili? This applies to both men and women.
Uzuri wa ndani unaitwa wema; nazungumzia uzuri wa nje. Wanaume hatuvutiwi na uzuri wa ndani kwanza mara nyingi kinachotushika machoni ni uzuri wa nje (maumbilie, sauti, macho n.k). Hivyo, mwanamme mwenye akili timamu hawezi kumchukua binti ambaye ana umri wa balehe ambaye akikaa na mke wake watu wanamuangalia yeye na si mkewe! Na yeye mwenyewe anamuangalia huyo kuliko mkewe.
I'm dead serious on this. Usimletee mke wako mashindano ya attention. I have been there.
2.Hawa wasichana siyo wajinga kama watu wanavyodhania. Mke na mume kwa vyovyote lazima wanaweza kuwa na mapungufu yao, na msichana huyu anasoma mchezo wote unavyokwenda na ata capitalise on the weaknesses za mke...... sasa ukisema usiajiri aliye mwema kuliko mkeo mhhhh!!??
Maandiko yanasema mke mwema hutoka kwa bwana haisemi hausigeli mwema! Hausigeli wako akiwa mwema kuliko mkeo muoe!
3.Bold 3, Huu ni mtihani.Kulala ndani na kuwa na sifa a u b.... hizi ndizo sifa ambazo humfanya hausigel aajiriwe! In short bold 1,2,3 huwa ni vigezo vya kumwajiri msichana.Hakuna mtu ataajiri msichana mkatili, asiyekuwa na sifa zozote aje amlelee watoto!u hausgel ni kazi jamani lazima iwe na vigezo.
To tell you the truth watu wengi wanaajiri wasaidizi wa ndani kwa ajili ya kile kinachoitwa "kazi za ndani" mambo ya kupiga deki, kusafisha vyombo, kufua n.k Haya mambo baba na mama mwenye nyumba wanaweza kuyafanya pasipo kuonekana kituko.
Leo hii kila mtu akifanikiwa kidogo tu anataka kuwa na msaidizi wa ndani! Hii ni mentality ya kikoloni! Watu wanatakiwa kuwa na msaidizi wa ndani pale ambapo wao wenyewe kwa namna fulani hawawezi mambo fulani hasa kusimamia watoto wadogo wakati wao wenye nyumba wanaenda kazini. Wenye nyumba wakirudi msaidizi anatakiwa aende zake kwake.
kwanza siamini katika kumuajiri mtu kwa masaa 24! kwa kisingizio cha kumpa pa kula na pa kulala. Kama kweli watu wanaamini hivyo wawapangie hao wasaidizi wao vyumba vyao.
Hili ni muhimu kwa sababu, wakati tunafikiria mahitaji ya mume na mke ya ngono tunaignore mahitaji ya ngono ya hao wasaidizi. Mnataka akae humo ndani kama mtawa wakati kuna mwanamme!?
4. Bold 4 ...hii nadhani ndio hasa chanzo cha tatizo - wanaume wengi wakware hujaribu kumvua mwanamke yeyote kwa mawazo/fikra na si ajabu kufanya hivi kwa hausigeli.
Hii si sababu ya ukware wala nini; mwanamme/mwanamke ni mwaminifu kwa kadiri ya chaguo lililo mbele yake. A man or a woman is as faithful as the options available to him/her.