Ila ukishajiita au kuwa cute tayari Kuna vitu vinakuwa haviko sawa!jamii inapambana kuhakikisha Binti anakuwa salama we unakuja na gender
Hoja hii tulishaijibu kwamba, jambo hili lipo kisaikolojia zaidi.
Watu huwa hawapendi mtu mwingine awaye yote kumzidi yeye kufanya jambo lolote ambalo yeye hulifanya.
Ndiyo maana mtu mwizi akisikia kuna wizi umetokea ama mwizi kakamatwa, anakimbilia kuuliza kachukua ama kaiba nini?
Mzinzi naye hivyo hivyo, kama kuna mtu kashikwa ugoni utasikia anauliza: 'yaani kakamatwa naye wakifanya kabisa, mimi siwezi kukubali'.
Watu wote wanaofuatilia jambo hili siyo kusema kwamba wote ni raia wema.
Wengi wao wanauliza ili wapate majibu ya kujengea jaziba zao zipande ili wakasirike watukane kupata afueni.
Mgoni huuawa na mzinzi.
Mwizi huuawa na wezi.
Mpokea rushwa hufungwa na hakimu mla rushwa.
Wazinzi wamekasirika Tz nzima si kwa sababu hao wabaka wamehoroganya tu maadili peke yake hapana, ni kwa sababu wenzao hao ni next level, wamefanya uzinzi wa kufuru, lazima hawa roho ziwaume sana.
Ndiyo maana Yesu alipangua hasira za wote waliotaka kumburuta kahaba kwa kisago: ... 'yayote ambaye hajawahi kutenda dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe'... Hakuna hata mmoja aliyethubutu, haooo wakatawanyika.
Kiukweli kila mmoja wetu akijiangalia kwenye kioo cha ndani ya roho yake ni mashudu. Ila kupaza sauti kulaani litokeapo jambo kama hilo ni lazima ila si kwa sifa za usafi wetu.