Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
‘Wanaume ni kama wanyama kihisia. Hawana huruma, hawajali na ndiyo maana hata kwenye msiba, unakuta wala hawaoneshi huzuni. Kwa kawaida hawajali kabisa, ni kama vile hawakuumbwa na roho.' Haya ni maneno ambayo yanatamkwa na mwanamke ambaye anaamini kwamba wanaume hawana hisia. Lakini siyo mwanamke huyu tu peke yake ambaye anaamini kwamba, wanaume hawana hisia.Kwa mfano, wanazungumzia sana kulia na pengine hata kucheka, kwamba, mara nyingi wanaume huwa wagumu kulia na hata kucheka kwao ni kwa kujikagua kwanza. Ndiyo maana unaweza kukuta wanaume wanaamini kwamba, kucheka sana kuna maana ya umwanamke au kwa mwanamke kucheka sana, kuna maana ya umalaya.
Wanawake hufurahia kucheka sana wakati wanaume huogopa kucheka sana. Katika hali fulani, watu wengi wanaamini kwamba, wanaume hawana uwezo wa kuonesha hisia zao kirahisi. Lakini ukweli unaonesha kwamba, wanaume na wanawake, wote wana hisia sawa, bali wanaume huonesha zaidi hisia ambazo zinawaumiza wenyewe na pia hisia ambazo zinaumiza watu wengine.Imethibitika kwamba, wanaume huwa wanatumia muda mwingi kufikiria mambo mabaya kuliko mazuri, hivyo hisia wanazopata mara nyingi ni mbaya. Wanaume huwa wanashiriki hisia zao na watu wachache sana.
Wanaume hujikaza kisabuni kwenye mambo yanayowaumiza. kusema hisia zao kwao ni kama udhaifu. Lakini hata wanapoelezea hisia zao, hawazielezi kwa njia yenye kugusa sana. Hutumia lugha ambayo haioneshi hisia na hata maneno yao pia siyo ya kihisia hasa. Lakini pia wanaume huwa hawasemi hasa hisia zao za ndani. Wanazielezea lakini husielezea kidogo au kwa kiwango ambacho sicho, yaani cha chini kuliko ilivyo. Wanaume mara nyingi wako tayari kuelezea hisia ambazo zinaonesha haja ya kudhibiti au madaraka ama nguvu. Kwa mfano, zenye kuonesha majivuno, hasira na kijicho, amri na kebehi. Wataalamu wengi wanasema wanaume wamefundishwa na jamii kuficha hisia zao, jambo ambalo huwaumiza sana bila wenyewe kujua.
Kwenye suala la hisia mwanamke na mwanaume wanaishi dunia mbili tofauti. Kwa hiyo siyo kweli kwamba, wanaume hawana hisia au hisia zao ni kidogo. Ukweli ni kwamba, wote wana hisia, bali wanaume hawana uwezo wa kuzionesha, wanazikandamiza wakati wanawake wamewezeshwa kuzionesha. Kuficha hisia hata hivyo kunaelezwa kwamba, huwa zinawaumiza sana wanaume kuliko inavyofikiriwa. Ndiyo maana kukiwa na vurugu kwenye ndoa, ambazo hutoa maumivu sawa kwa mwanamke na mwanaume, mwanamke anaweza kuwa na nafuu kubwa kwa sababu atasema hisia zake na atakuwa amepunguza kuumia kwa mwili.
Kwa mwanaume mara nyingi maumivu yanakuwa makubwa kwa sababu hukandamiza mengi ambayo baadae huja kumuumiza kimwili.Ni kweli kwamba, vurugu za ndoa huwaumiza wanawake zaidi, lakini kama ni vurugu ambazo mwanamke na mwanaume wanabeba mzigo sawa, mwanamke anakuwa kwenye nafuu zaidi kwa sababu ya uwezo wake wa kusema hisia zake na hivyo kuweza kupunguza maumivu.