Uporoto01, ni kweli yanakuwepo maongezi baada ya date....ila bado nafikiri msichana aliyekomaa zaidi hahitaji kupata approval ya rafiki. Unaweza ukaenda na rafiki kwenye date yako..then akakushauri mkaka hafai..kumbe yeye kampenda...ohhh!!! yapo hayo.
About my name...hili jina ninalipenda.... ni jina la mmoja wa mabinti wa Ayubu (kwenye biblia)..likiwa na maana "horn or child of beauty". I just like the name....
Hapo huyo dada kafanya makosa matatu makubwa (she committed 3 grave mistakes):
1. Kuharibu miadi ya jamaa (she spoiled the date). Yaani unaalikwa mpate muda wa kuongea na kufahamiana halafu wewe unaanza kubeba ndugu na ukoo mzima?
2. Kuomba omba hela na lift
3. Kuonesha kuwa hata huko mbele atakuwa yeye ni wa wakupokea tu (recipient) na huyo mwanamume atakuwa mtoaji tu (donor)
Kwa hiyo huyo dada ameonesha tabia za kiswahili na za kizamani, hastahili kupewa nafasi!
I'm glad dearest!!Heheheheheh!!!Aisee inabidi nikuweke ndani....don't be using shem like that bwana!!!
Yani babu wajukuu wasipobadilika hutapata wakwe kabisaaaaaa!
Wanaume kweli sio ATM na mkielemewa mseme!!!...kweli kama nikienda date na shosty wangu ujue namzingua jamaa vinginevyo napenda date iwe na maana yani mtu mbili tu!!
Mimi nakubaliana na V of R kuwa sio vibaya mwanamke akija na shoga'ke kwenye date ya kwanza ili aweze kusaidia kumthaminisha jamaa aweze kumshauri baadae kama atamfaa baada ya hapo inabidi aje peke yake lakini hili la vocha kila kukicha alafu hapigi inaboa na mwimbaji MR.Paul aliimba kwenye wimbo 'dola kumi kila simu waishia kunibipu wampigia nani' ?
Ndo nilivyofundwa jamani, will change my dear....ila halalamiki sasa wala hasemi hana ye nikimuomba ananipa tu kwa furaha.....:laugh::laugh:
Yeah ni ngumu kumvumilia mtu wa aina hiyo kama wewe hujazoea!Wapo wengi tu, tunapata na tutaendelea kupata. Unajua hii dunia, kila shetani na mbuyu wake. Kuna wanaume pia wanapenda sana kuombwa omba vitu kama hivyo na hiyo hali inawavimbisha kichwa. Kwa maani hiyo, msichana kama huyo atakuja kupata mswahili swahili mwenzake. Ila kama ni mimi, sina hakika kama hiyo dinner tungeimaliza pamoja.
Yeah ni ngumu kumvumilia mtu wa aina hiyo kama wewe hujazoea!
Hehehehe!Nimekusoma dearest!Hata hivyo kama unampenda na uwezo wa kukupa anao then humtumii so it's owkey!Ila kama unamchezea tu ntakuchapa!!Lolz
Kweli babu!Mwenyewe niliboreka kweli huyo kaka aliponieleza!Ila angalau amemjua mapema kabla hajapoteza muda na pesa kutengeneza uhusiano ambao hautadumu wala hatafurahiaNdo maana nmashauri huyo kijana asikae tena akamwaza au kumpa nafasi huyo dada. Ni mjinga tu na hajui atokako, aliko na anakotaka kwenda. Wakati huo huyo kaka anatafuta mwenza wa maana ili waanze maandalizi ya maisha. Huyo msichana hayuko kati ya wale wanaomfaa.
Nimekereka kwa kweli!
Babu DC
Kweli babu!Mwenyewe niliboreka kweli huyo kaka aliponieleza!Ila angalau amemjua mapema kabla hajapoteza muda na pesa kutengeneza uhusiano ambao hautadumu wala hatafurahia
Kwa mtu yeyote makini, huyo dada ni bomu linaloweza kukulipukia wakati wowote. Lazima utimue mbio haraka sana.
Ila limenijia swali moja la kipuuzi. Hivi wewe umeanza anzaje kuwa na urafiki na mtu mpuuzi kama huyo dada? Sorry kama nimekukwaza!
Hahahahaha!Wala hujanikwaza!Huyo rafiki yangu wa kiume nae aliniuliza hivyo hivyo!Newayz nilimwona mzuri kabla sijamsoma!Nimeshaanza kumpotezea sasa!
Ni kweli ila wanaume wengine wao wenyewe ndio wanajiwekea mazingira ya kuchunwa chunwa. We mmekutana siku ya kwanza anakuelezea assets zake zote majivuno ndio usiseme.
Aaaaargg sijui wanafikiri ndio watapata wapenzi kirahisi!
Wengine huwa hatuwezi kuomba omba ila mwanaume wa hivyo akikutana na mwanamke mcharuko atachunwa hadi basi.