Wanaume tabia hii ya asili inawaumiza wanawake(hit and run)

Wanaume tabia hii ya asili inawaumiza wanawake(hit and run)

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
21,859
Reaction score
19,736
First impression unamuwaza, unatamani ungepata nafasi penzi lako lote ulimalizie kwake,yaani hapa hata ATM card unaweza submit kwake. Ukishatupia swaga zako, kwa kujifanya very romantic, mtoto anakusikiliza unapima upepo unaona hapa niongeze nguvu fasta fasta plan za kula, bila kupoteza nafasi unageuka Messi ndani ya 6 box anakufunulia unakiona kile ulichokua unakijengea "image".

Sasa hapa ndio ulipomtihani na matarajio ya wanawake wengi,upendo ndo milango yake inakua imefunguka (kisaikolojia inasemekana mwanamke ndio anaanza kupenda) lakini kwa upande wa wanaume anakua ameshamaliza shughuli zamani kama hajaridhika hata angekua Miss World huyo msichana.

Mwishowe mwanaume anaweza kujilazimisha akarudia mara mbili,t atu ghafla mwanaume anaanza kubadilika kabisa no text ,no calls ,no transactions etc(hapa ndo utakuja kuamini kwanini dini, jamii nyingi zamani waliharamisha ngono kabla ya ndoa) tofauti na matarajio ya Dada ambaye ndo anakua kwenye page za mwanzo za "kitabu cha historia ya mapenzi yake".

Tafadhalini sana akina dada wasaka ndoa usijisikie vibaya sisi ndo tulivyo na nakuhakikishia inawezekana ukawa na ubora 100% sema tu tamaa ndo ilimfikisha hapo huyo mwanaume.Usikate tamaa wasiwasi wangu hata atakapokuja the destinied husband (soulmate) wako ambaye atakupenda unconditionally atakuja na style kama ya huyo jamaa aliyekukatisha tamaa akakubakiza na makovu.

Je mwanamke kama huyu atam trust mwanaume mwingine? Hapo ndo ule usemi unakuja "All men are the same" however who told u to test them. Ushauri wangu usikate tamaa you should always expect for good your marriage is nearly coming,huyo mtu aliletwa ili upate somo la kumpenda mumeo na kumuheshimu siku utakapoolewa.

THATS THE WAY IT IS

Siku njema wakuu
 
Hivi siye huwa hatuhit na kurun...
Cc....fulani
 
usinikubali harakaharaka (mimi)...Fid Q
 
Na mimi nasema waliwe tu, wakat wanapewa mi'offer wanachekelea tu, there is no such thing as free in this world"
 
Tutakuita Malaya mtaani kote

CHAPA ILALE: ukinifuma napiga sound utajua mume si huyu?nipe uone napiga siku1 ya 2 ya 3 ya 4 simu haipatikani nmeshamaliza kazi yangu...Ahadi zote zinayeyuka.
 
Kwa hiyo unawashahurii madada zetu wasikate tamaa waendelee kutoa papuchi,
 
CHAPA ILALE: ukinifuma napiga sound utajua mume si huyu?nipe uone napiga siku1 ya 2 ya 3 ya 4 simu haipatikani nmeshamaliza kazi yangu...Ahadi zote zinayeyuka.

Dah!Ee mola uturehemu.
 
Tabia ya asili ya mwanaume kwa maana ya mwanaume si kuwachezea wanawake kwa kuwafunua tupu zao na kuwaacha...bali ni kuoa mwanamke mmoja na kupambana kuihakikishia familia yake inapata mahitaji yote ya msingi...hizo tabia za kuwavua chupi wadada na kuwaacha ni wavulana walio kwenye balehe...au hufanywa na wanaume waliokuwa miili na vimo ilhali akili na fikra ni za kivulana............
 
Tabia ya asili ya mwanaume kwa maana ya mwanaume si kuwachezea wanawake kwa kuwafunua tupu zao na kuwaacha...bali ni kuoa mwanamke mmoja na kupambana kuihakikishia familia yake inapata mahitaji yote ya msingi...hizo tabia za kuwavua chupi wadada na kuwaacha ni wavulana walio kwenye balehe...au hufanywa na wanaume waliokuwa miili na vimo ilhali akili na fikra ni za kivulana............

Na waume za watu wanasifika kwa kuhonga nao ni wavulana?
 
Na waume za watu wanasifika kwa kuhonga nao ni wavulana?
Kwanza tambua kuwa unapomtaja mwanaume..ujue unamzungumzia mtu aliyekomaa kifikra...ujue unamzungumzia mtu ambaye anajua anatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani...unamzungumzia mtu ambaye ni kichwa cha familia au kiongozi wa familia kwa hiyo lazima awe na maono na akili iliyokomaa ili aweze kuiongoza vyema familia yake....mwanaume mwenye fikra pevu hawezi akasimama mbele ya umati na kujigamba kwa kuwahonga wanawake wa nje hali ya kuwa anajua kuwa hatima ya ustawi wa familia yake iko mikononi mwake...

.mwanamume mwenye utimamu wa akili hawezi akakaa sehemu za starehe na kufuja fedha hali ya kuwa familia yake inateseka kwa kukosa mahitaji muhimu......mwanaume aliye timamu hawezi kuyumbishwa na matamanio ya kimwili kwani anajua kuwa nyumbani yupo malkia wake mwenye jukumu la kumtimizia haja zake.....matendo ya kuwafunua wadada na kuwaacha huwa yanafanywa na wanaume wanaoonekana kuwa ni wanaume hali ya akili zao na maamuzi yao vinaongozwa na matamanio...hawana tofauti na wavulana wanaohangaishwa na balehe na ugeni wa mambo...

..ni matukio ambayo hayana faida kwa mwanaume zaidi ya hasara kwani huyumbisha uchumi wake.....wengi wa waliokuwa na tabia hizo nikiwa na maana ya kuwekeza rasilimali zao katika kuwafunua wadada vyupi vyao na kuwaacha wanaonekana kujutia kwani mwisho wa siku hakuna faida badala yake wanahesabu hasara.....kitu ambacho baadhi ya wanaume hawakijui ni kwamba wanawake wazuri hawaishi na kamwe hawajawahi kuisha hapa ulimwenguni kwa maana ya kuwa kila siku wanazaliwa wapya na wazuri kushinda uliowaona mwanzo....na wanavutia haswa kwa kuwa wao ni mapambo ya ulimwengu.....busara ni kuoa.....na hekima ni kutulia na mkeo....
 
Back
Top Bottom