Wanaume tujipende, uchafu sio deal, kataa kuwa mchafu

Chrismoris

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Posts
14,113
Reaction score
17,645
Natumaini mmeshasalimiwa sana tangu asubuhi hadi mmechoka.

Ok mchongo wa leo ni kuhusu Usafi au umaridadi au utanashati.

Wakulungwa tujipende wazee,
kuwa msafi haimaanishi unapoteza "uanaume" wako,

Usafi haujalishi unavaa nguo za pesa ngapi wala mambo ya marashi marashi bali wakati wote zingatia usafi wa kinywa, mwili na mengineyo.

Kuwa 'broke' haimaanishi kuishi katika uchafu, Au sio masela?

Wahenga wanasema umaridadi uficha umaskini Peace and love , tuwe wasafi bwana.
 
Nmeamini kweli wanaume tumebaki wachache.

Eti huyu nae ni mtoto wa kiume
 
Nani amekwambia sisi ni wachafu
Jibu haraka kabla hatujakuchukulia hatua mwkt wetu wa chama cha wanaume tanzania ujumbe umemfikia yaaani niende kufyatua matofali ya udingo na suti
 
Inategemea na nature ya kazi ya mwanaume husika.
Fundi gereji, muuza mkaa, fundi ujenzi, seremala, fundi bomba, mtapisha vyoo et.c . Anaanzaje kuwa msafi muda wote?
 
Usafi ni tabia mkuu kama zilivyo tabia zingine kama.
Ulevi.
Kuvuta sigara,
Kupenda chini.
Kwenda club,
Nk.
Yupo mtu ana suruali moja na t-shirts 2, lakini kila muda ni msafi na ananukia perfume safi kabisa..
Yupo mtu ana pesa na ana nguo nyingi na viatu vingi lakini vyote anavaa vikiwa vichafu,,bila pasi..hata deodorant ya 5000 inamshinda,,,na anajionea sawa tu..
Usafi na utanashati ni tabia kama tabia zingine.
 
Umaridadi bila hela ni sawa na kuwa tajiri kama Bill Gates ila upo hoi na cancer kitandani.
 
Una undugu na yule jamaa aliesema wanaume mkioga mpake mafuta kwenye makalio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…