Wanaume tukome kuwekeza kwa mahawara!

Hapo kwenye red:Bishanga abbashaija!Kweli ndugu yako hana maana.Na hao wadada wanaopenda vitu vikubwa ni hatari hakimaliza tu kununua hivyo vitu na penzi ndo kwisha kabisa.

Mkuu hapo hujajumlisha na gharama za pango alilomlipia,renovations,kufunga AC,kukata leseni....we acha tu...hawara gharama.
 

Nilifikiri ikiwa lipustiki ya bei mbaya unaruhisiwa!!!

Lol@haki-ya-paw
 
Kama ni hivyo basi muhakikishe na mradi wa kuku nyumbani haufi.

jamaa hana njia itabidi ajikunje tu katika hilo ingawa sms kairuka kimanga,ila sasa sijui itakuwaje shemeji atapompigia simu huyo mdada au si ajabu keshampigia.
 
Ingekuwa mie ndio huyo maza hous, wala nicngetoa povu la hasira, ningechat na huyo kimada na kupanga na huyo wapi tuonane kesho yake ili achukue pesa, atajua anawasiliana na malaya mwenzie na atakuja.

Nitacopi namba zote za jamaa kwenye line yangu icpokuwa ya huyo malaya wake na kuiweka kwenye simu yake na mie nachukua line yake najua itachukua mda kugundua na atakuwa kazini na mie namfata huyo bidada c unajua mwizi akikamatwa lzm afate mashart kwa style yangu lzm atanipa ushirikiano na tutamweka kati huyo bwana.

Na kumwita aje na kujibu tuhuma tena mbele ya mashahidi wa ukweli, naamini itakuwa mwanzo na mwisho wa umalaya wao na atajua umuhimu wa mkewe na wanae, ni mawazo yangu tu.
 
Bishanga unataka kutwambia ulikuwa hujui ya huyu mdogo wako au umechukia kwa kuwa kabambwa?
 
Kwa kweli wanao fanya haya hasa huwa ni wame za watu siku ukiwa huna kitu kwa hao mahawara unapisha wenzio wenye nacho waendeleze kula vyombo wanawake wengi wa nje wanaangalia pochi yako tu coz hawahitaji kupiga picha na wewe ipo siku na yeye huyo mwanaume ataumizwa mara mia ya anavyo muumiza mkewe.

Nimeona sana wanaume wa stly hiyo huwa mwisho wao ni mbaya na huishia kupata haibu tu kwa jamii . Hembu jaribuni kuwaambia hao mahawara umepata tatizo na mambo yako ya kifedha hayaendi vizuri uone nakupa week tu utapata majibu hakuna cha baby wala swtheart utasikia tu ili nalo lisumbufu na utaishia kutopokelewa simu kabisa . Cha muhimu tulieni kwenye ndoa jamani unaepuka mengi sana
 
Ila sio haya bana mengine ni ya kujitakia kabisa
We mkeo na watoto wanallalia dagaa nyumbani kama msosi ila nyumba ndogo inakula kuku

too sad lakini mabo haya ni very common mitaani.
 
Hii topic imenikumbusha vituko vya baba yangu. Baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara. Kwa hiyo alikuwa anajulikana sana kwenye mabenki, those days ni hizi benki za serikali. Sasa alikuwa hajatulia though yeye alikuwa a bit smart in a sense hakuwa na hawara ambaye anaweza kujiita nyumba ndogo ni alikuwa ni kind of hit and run.

Sisi tulizaliwa wengi (wote mama mmoja baba hakuwahi kuzaa nje). Mama alikuwa akisafiri baba analeta wanawake ndani akitoka kwenye pombe zake. Kuna kipindi alikuwa anamleta mdada mmoja mfanyakazi wa benki; those days wadada wa benki walikuwa warembo sana na walikuwa wanapenda saaaana ma sugar daddy. Sasa kwa kuwa dingi alikuwa corporate customer alikuwa anawapata kirahisi.

Ndugu zangu wakaweka kikao (mimi nilikuwa mdogo sijuhi std two vile wao walikuwa a bit old, walikuwa secondary) Wakapanga kuwa baba akimleta hawara yake wamfundishe adabu.

Baba yangu hajawahi kulala nje nadhani ndio maana alikuwa anaamua kuwaleta wanawake ndani afu wanaondoka asubuhi sana kama walinzi, na yeye alikuwa ana imani kuwa hatumuoni kwani alikuwa na funguo zake na geti alikuwa anafungua mlinzi.

Siku moja karudi na mwanamke wake kama kawaida yake dada zangu na kaka zangu walikuwa wamejificha kwenye maua na fimbo zao; walishamsoma akiingia anamshusha huyo mwanamke , afu yeye anaingiza gari garage, ndio wanaingia wote ndani. Ile anaingiza gari garage wacha ndugu zangu waibuke na kuanza kumtandika yule mwanamke. Alipiga makelele, nadhani pombe zilimtoka. Ilibidi baba achukue gari alimrudishe yule dada. from that day hatukuwahi kuona mwanamke yeyote home na baba hakuongea kitu.

Mama alivyorudi wote tulikaa kimya hatukumwambia what happended.

Hope none of my bro or sis is JF member. Maana atacheka saaana.
 

hii ni hatari jamaa anaweza kudondoka afe.
 
hivi na wewe ni nyumba ndogo wa desh deshi eeh?
Hahahaha! Naogopa dhambi jamani..lol watoto wale dagaa afu mimi ninunuliwe draya?..khaaa sio laana ni nini husni? Jiulize hv je kama ndo mimi watoto wangu wanakula dagaa ntafurahi? Hizi nyumba ndogo hizi, zipo kwaajili ya raha tu, nyumba kubwa ndo za kuvumilia shida! Mume akisema wife nimeishiwa mwezi huu itabidi unihelp kulipa skuli bus, tunaitika sawa mume wangu, kumbe mwenzio hajaishiwa wala nini, hela zipo ila hazitoshi kugawana na hawara..
 

ni dhambi sana kutesa watoto wa mwenzio na mwanamke mwenzio kwasababu ya maslahi binafsi.
Wanaume acheni kutafta mahawara.
 
ni dhambi sana kutesa watoto wa mwenzio na mwanamke mwenzio kwasababu ya maslahi binafsi.
Wanaume acheni kutafta mahawara.
Toka nijiunge jf leo ndo nimeona umechangia kwa moyo wako wote tena ukimaanisha.. Utanidai thanks yako 1 kwa hii useful comment yako, siku mods wakirudisha thanks nitakugongea!
 
hii hali inatishia maisha sana .... sijui hakuna mawazo endelevu au inakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…