Hii topic imenikumbusha vituko vya baba yangu. Baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara. Kwa hiyo alikuwa anajulikana sana kwenye mabenki, those days ni hizi benki za serikali. Sasa alikuwa hajatulia though yeye alikuwa a bit smart in a sense hakuwa na hawara ambaye anaweza kujiita nyumba ndogo ni alikuwa ni kind of hit and run.
Sisi tulizaliwa wengi (wote mama mmoja baba hakuwahi kuzaa nje). Mama alikuwa akisafiri baba analeta wanawake ndani akitoka kwenye pombe zake. Kuna kipindi alikuwa anamleta mdada mmoja mfanyakazi wa benki; those days wadada wa benki walikuwa warembo sana na walikuwa wanapenda saaaana ma sugar daddy. Sasa kwa kuwa dingi alikuwa corporate customer alikuwa anawapata kirahisi.
Ndugu zangu wakaweka kikao (mimi nilikuwa mdogo sijuhi std two vile wao walikuwa a bit old, walikuwa secondary) Wakapanga kuwa baba akimleta hawara yake wamfundishe adabu.
Baba yangu hajawahi kulala nje nadhani ndio maana alikuwa anaamua kuwaleta wanawake ndani afu wanaondoka asubuhi sana kama walinzi, na yeye alikuwa ana imani kuwa hatumuoni kwani alikuwa na funguo zake na geti alikuwa anafungua mlinzi.
Siku moja karudi na mwanamke wake kama kawaida yake dada zangu na kaka zangu walikuwa wamejificha kwenye maua na fimbo zao; walishamsoma akiingia anamshusha huyo mwanamke , afu yeye anaingiza gari garage, ndio wanaingia wote ndani. Ile anaingiza gari garage wacha ndugu zangu waibuke na kuanza kumtandika yule mwanamke. Alipiga makelele, nadhani pombe zilimtoka. Ilibidi baba achukue gari alimrudishe yule dada. from that day hatukuwahi kuona mwanamke yeyote home na baba hakuongea kitu.
Mama alivyorudi wote tulikaa kimya hatukumwambia what happended.
Hope none of my bro or sis is JF member. Maana atacheka saaana.