Wanaume tuliowahi kupigwa na wanawake tukutane hapa

Wanaume tuliowahi kupigwa na wanawake tukutane hapa

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Kuna wanawake wakorofi bhana. Tena ukorofi unawazidi pale wanapojua huyu hawezi kunipiga.

Na wanaume tunavyojua kutunza siri ukipigwa hupigi kelele majirani wasije wakaskia...unajikalia kimya yaishe kesho kupambazuke.

Nilishawahi kuwa na mwanamke nikawa nampuuza. Anapiga simu sipokei, ananiita sehemu namwambia nipe dakika tatu kisha sitokei. Sasa siku nikammiss nikamwita akaja siku hiyo akaja na pombe zake nadhani alinipania maana hanywagi...zilipokelea akaanza na tukofi twa mahaba nikajua anatania.

Eeeh bwana nikampuuzia akaja akanipa moja ilibaki kidogo nimuue ila hasira zikashuka fasta. Hakuacha akajua huyu hawezi kujibu. Na kiukweli siku hiyo sikujibu nikawa namzuia tu asinipige...ila alikuwa mkorofi...sijui kaacha tabia zake.

Wanaume tunachezea saana sema hatuyasemi nje.
 
😂😂 kumuachia kiboya hivyo itategemea nina nini kichwani!! Akikuta awamu ya tano imenivuruga lazima aite majirani kumnasua!!
Mkuu hata hivyo ilikuwa Ni haki yako ulizidi uongo Tena angekutoa na ngeu ikawa Kama kumbukumbu..
 
[emoji23][emoji23] kumuachia kiboya hivyo itategemea nina nini kichwani!! Akikuta awamu ya tano imenivuruga lazima aite majirani kumnasua!!
Mkuu hata hivyo ilikuwa Ni haki yako ulizidi uongo Tena angekutoa na ngeu ikawa Kama kumbukumbu..
Sasa unapiga mtu ambaye unajua unauwezo wa kumpiga mkuu?

Halafu wanawake mkigombana hajishughulishi hata na wewe ukumpiga tu anaangukia vitu vya thamani....nikaona kuepusha gharama acha nimwache.

Sio uongo....Fanani alifeli hadhira nikalala.
 
Nina weakness ya kupiga kiumbe cha kike hata n'gombe jike simpigi...namkinga asiniumize tu.
Mi navyojua wanavosema mwanamke hapigwi, humaanisha kua akikuudhi kwa maneno yake au majibu yake. Na ndio maana wanasema mke hupigwa kwa upande wa kanga

Sidhani kama walimaanisha kua akikupiga we umuangalie tu,
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa unapiga mtu ambaye unajua unauwezo wa kumpiga mkuu?

Halafu wanawake mkigombana hajishughulishi hata na wewe ukumpiga tu anaangukia vitu vya thamani....nikaona kuepusha gharama acha nimwache.

Sio uongo....Fanani alifeli hadhira nikalala.
Wanawake wasumbufu kama hao unakafunga kamba mikono na miguu, and then unakaweka kwenye kenchi.
 
Back
Top Bottom