Duh,.. mie kuna msichana aliiteka akili yangu kwa kutaka kujua ratiba yangu ya kazi ikoje. kwa hiyo kila nilipomwambia kua natoka kazini kulekea home alikuwa ananiambia "pole" wakati huo hatukua na uhusiano wa kimapenzi halafu mimi nilikuwa bado si mwenyeji sana hapa Dsm. kw hiyo alipokua ananiambia pole basi najiona mtu wa maana na nikifika nyumbani ananiambia "jitahidi ule kijana" yaani niliona kuwa ndiye mtu anaenijali kuliko hata mama mzazi. kwa kua nilikuwa mgeni jijini alikuwa karibu nami kimawasiliano na baadae tukajikuta tumeanza mahusiano